• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Jaji Rumanyika atoa maagizo kwa mahakama akizindua Mobile Court

Posted on: July 10th, 2019


Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imezindua  rasmi  gari la mahakama inayotembea (mobile court) jijini Mwanza kwa lengo la kuisaidia usikilizwaji wa mashauri  Mkoa ya Mwanza   ambapo itaweka kambi maeneo la Buhongwa, Buswelu na Igoma.

Uzinduzi huo ulifanywa  na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Sam Rumanyika ambapo alisema  matumizi ya mahakaa hiyo ni ya kisasa  zaidi katika kusogeza huduma karibu na wananchi iliyopewa kauli mbiu ya “Niruhusu niseme mlangoni, mpe raha mteja mahakama ing’are”.

Jaji Rumanyika   alisema gari hiyo ya kidijitali kwa  mahakama itawapunguzia wananchi gharama na muda wa kutafuta haki mahakamani ambapo aliitaja jamii hasa wanawake  kuchangamkia fursa hiyo.

“Kila ninapotafakari ujio wa aina hii ya mahakama katika kanda ya Mwanza naona ni kiwango cha bahati sana ukizingatia magari kama haya yapo mawili tu nchini, moja limebaki Dar  es Salaam kwa ajili ya maeneo ya Kibamba, Bunju, Chanika na Buza, hivyo ni fursa ya kipekee kwetu.

“Inabidi tuchangamke kweli na tufikie mahali kama ikiwezekana yale mashauri yanayotokana na operesheni za uvuvi, uwindaji haramu yaletwe katika vituo vilivyopangwa na kutashughulikia haraka, kuna mashauri ambayo yataisha kwa siku moja na kutolewa hukumu.

“Tukumbuke kuwa katika takwimu zinaonyesha katika mahakama za mwanzo ndipo takribani asilimia 70 ya mashauri husajiliwa kila siku nchini nzima, hivyo siyo mbaya gari hili likaelekezwa kutoa huduma huko,”alisema Jaji Rumanyika.

Hata hivyo Mhe. Jaji Rumanyika aliwahimiza  majaji na hakimu wa mahakama mbalimbali kanda ya Mwanza kuwahudumia kwa uharaka na kwa haki wananchi ili kuokoa muda wao na kwenda kujitafutia riziki na kujenga uchumi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Aliwataka majaji na mahakimu  kutoa nakala ya hukumu ndani ya siku saba au papo hapo ingawa sheria zinaelekeza kutolewa ndani ya siku 21 ili kuondoa malalamiko yaliyopo ya ucheleweshaji na kusisitiza kuwa mtazamo wake ni kuona mahakama zinakuwa ‘fast track’.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella alisema  ujio wa gari hilo linalotembea kutoa huduma za kimahakama linapaswa kutumiwa vema na watumishi wa sekta ya kisheria ili kuleta mabadiliko chanya.

Mhe.Mongella alisema  hivi sasa hajapokea malalamiko mengi kutoka mahakama kuu juu ya kucheleweshwa kesi zao isipokuwa wananchi wengi wanalalamikia katika mahakama za mwanzo, hivyo aliomba kama ikiwezekana nguvu kubwa ielekezwe huko.

 Ilielezwa kuwa gari hilo hadi kukamilika kwake limegharimu Sh milioni 470.8  huku likiwa na Televisheni, kamera zenye uwezo wa kurekodi ushahidi wote kwa picha na sauti, lifti kwa ajili ya watu wenye ulemavu na kipaza sauti kwa ajili ya kutangaza ratiba ya mahakama hiyo.

Itakumbukwa, Rais  Dkt. John Magufuli alizindua gari hizo za mahakama inayotembea Februari 6, mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya sheria kwa ajili ya kutoa huduma ya usikilizwaji wa mashauri katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.