JENGO JIPYA LA KISASA LA HUDUMA YA MAMA NA MTOTO LAZINDULIWA HOSPITALI YA SUMVE
Katika kujenga uhusiano bora wa kidemokrasia Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umeendelea kusaidia na kuboresha miundombinu katika Sekta ya Afya
Akizindua Jengo la kliniki bora na ya kisasa Balozi wa Japan nchini Mhe. Yasushi Misawa amesema ubora wa Jengo hilo uendane na ubora wa utoaji huduma kwa wananchi hususani Mama na mtoto.
Ameongeza kuwa sanjali na miundombinu ya kisasa wahakikishe wanalitunza na kutumika kwa muda mrefu ili kupunguza vifo vya Mama na mtoto.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amesema uwepo wa Jengo hilo la kisasa utasaidia ubora wa huduma kwa jamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.