KAMA TUNAHITAJI KUSONGA MBELE NI LAZIMA KUJIUNGA NA USHIRIKA – RAS BALANDYA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Balandya Elikana amewataka Maafisa Usafirishaji na Wadau wa Usafiri na Usafirishaji Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanajiunga na vyama vya ushirika kwa kuwa ushirika una mchango mkubwa katika uboreshaji wa maendeleo ya sekta ya usafiri na usafirishaji.
Katibu Tawala ametoa wito huo mapema leo Juni 24, 2025 wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Usafirishaji Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika Ukumbi wa Ghand Hall, Jijini Mwanza na kutaka Mkutano huo kujadili namna bora ya uendeshaji wa wa sekta hiyo kwa njia ya ushirika.
Aidha, Bwana Balandya amesema Dira ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona kuwa sekta ya usafirishaji nchini inakwenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia duniani hivyo kuweka msisitizo katika matumizi ya mifuno ya kidijitali kama mfumo wa tiketi mtandao.
“Kadhalika Serikali inahamasisha ushirika ili kuwawezesha wadau hawa kushirikiana, kupata mikopo kwa urahisi kuongeza nguvu ya sauti yao katika maamuzi na kutoa huduma kwa kuzingatia uweledi na ufanisi”. Katibu Tawala.
Ushirika ni muhimu sana, kama tunahitaji kupiga hatu kubwa na haraka ni lazima tujiunge na kuanzisha ushirika, ndio maana kuna msemo usemao kama unataka kufika mbali basi nenda na wenzako. Ameongeza Katibu Tawala Mkoa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu LATRA, DCP Johansen Kahatano Mkurugenzi wa Brabara LATRA amesema wamekuwa na utaratibu wa kukutana na Wadau wa sekta ya usafirishaji na kutoa elimu kwa kila mwaka na kuona namna ya kuwafanya wadau hao kuungana na kuwa wenye nguvu na kutoka kwenye usafiri mdogo kwenda usafiri mkubwa.
Aidha amesema lengo lingine ni kuhakikisha wanachochea uchumi wa mtu mmoja mmoja ili uweze kuwa mkubwa na kisha waweze kushiriki vyema katika huduma ya usafirishaji hapa nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.