WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt. Angeline Mabula amevunja kamati ya mipango mji ya jiji la Mwanza iliyokuwa mwenyekiti wa kamati ya Ardhi na mipango miji wa jiji la Mwanza Hamidu Said na mkurugenzi wa jiji la Mwanza Yahya Sekieti(katibu wa kamati).
Waziri Mabula ametoa maamuzi hayo magumu Jijini Mwanza wakati wa kikao kazi cha viongozi wanaosimamia sekta ya ardhi kwa ngazi zote kuanzia wilaya , mitaa, kata na mkoa.
"' Kamati zote za mipango miji na zile za uchumi, Serikali ni moja tumefanya mawasiliano na tunaenda kuchukua maamuzi magumu kwa ushauri pamoja na Waziri wa Tamisemi kamati ya mipango miji ya Jiji la Mwanza inaenda kuvunjwa na hakuna mjumbe hata mmoja atayetakiwa kurudi tena kwenye kamati Ile .'' Amesisitiza Waziri Mabula
Amesema katika mkoa wa Mwanza kumekuwa na tatizo kubwa la kudhulumu ardhi kwa wazee na wajane, na kuongeza kuwa kumekuwa na tatizo la utoaji vibali vya ukarabati wa majengo umekuwa unakiukwa sana.
Amezitaka Halmshauri zote nchini kutenga maeneo ya uwekezaji na kuyalinda kwa ajili ya kupokea wawekezaji.
''Suala la utatuzi wa mgogoro wa ardhi sio suala la Wizara eti kusema kuna mawaziri nane, nitashangaa eneo Lina mamlaka alaf mtu anasubiria Waziri, Mkuu wa mkoa au Mkuu wa wilaya, shughulikieni migogoro ya ardhi katika maeneo yenu".Amesema Mhe.Mabula
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amesema Kamati za ardhi zinashida sana na amemuomba Waziri Mabula kushugulika na wilaya ya Nyamagana kisha wilaya ya Ilemela.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.