Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa! Huu ni usemi uliozoeleka nchini kuelezea umuhimu wa sekta ya kilimo kwa maendeleo ya Taifa.
Mkuu wa Seksheni ya Uchumi na uzalishaji, Emily Kasagara anasema mkoa wa Mwanza umeendelea kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kufanya kilimo nchini kuwa cha kisasa, chenye tija na cha kibiashara.
Mafanikio tayari yameanza kuonekana katika na uzalishaji wa zao la pamba ambako Kasagara anasema umeongezeka kutoka tani 17,413.5 msimu wa kilimo wa 2017/2018 hadi tani 49,573.34 msimu wa 2018/19, ikiwa ni ongezeko la tani 32,573.34 sawa na asilimia 187.
Kwa upande wa usambazaji wa mbegu, anasema mahitaji ya mbegu za pamba kwa msimu 2018/19 yalikuwa ni tani 2,691.5, tani 2,585.52 za mbegu sawa na asilimia 96 zimesambazwa kwa wakulima, ambapo mbegu za manyoya za pamba ni tani 2,309 zilisambazwa kati ya lengo la tani 2,373.6 na jumla ya tani 276.5 za mbegu za kipara zilisambazwa kwa wakulima.
Hata hivyo anasema kutokana na mwenendo mbaya wa hali ya hewa, msimu wa 2018/19 uzalishaji wa chakula hasa aina ya wanga hautawezesha mkoa kujitosheleza kwa mahitaji ya aina hiyo kwa asilimia 100 na hivyo upungufu wa mahitaji ya chakula aina ya wanga unatarajiwa katika kipindi cha msimu wa 2019/20.
“Kwa sasa uzalishaji unaweza kutofikia matarajio ya mavuno ya tani 724,042.78 za mazao ya wanga,” anasema.
Kwa upande wa huduma za ugani, anasema hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu jumla ya wakulima 100,114 walikuwa wamepatiwa mafunzo ya kanuni bora za kilimo, ambapo Manispaa ya Ilemela ilitoa mafunzo kwa wakulima 428, Kwimba-45,200, Magu-23,005, Sengerema-4,826, Buchosa-21,752, Ukerewe-1,348, Misungwi-2,826, Jiji la Mwanza-663.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.