Serikali imekamilisha ujenzi wa vivuko saba zikiwemo Ambulance maalum tatu kwa ajili ya kusaidia usafiri katika mikoa mbalimbali hapa nchini vyenye thamani ya Sh. Bilioni 36.36.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano( sekta ya ujenzi) Elias Mwakalinga katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv.Ukara II hapa kazi tu.
Alisema kwa miaka mitano serikalli imejenga vivuko saba pamoja na Ambulance maalum tatu pia kwa sasa timu ya watalaam wake ipo mkoani kwa ajili ya kufanya utafiti ili kubaini maeneo yanayohitaji vivuko na kuyaainisha.
Pia alisema baada ya ajali Mv.Nyerere iliyozama September 20 mwaka 2018,ambapo watu takribani 227 walipoteza maisha serikali kupitia Wizara iliamua kununua kivuko mbadala chenye urefu wa mita 42 na upana wa mita 10 na chumba maalumu cha kujifungulia hiyo ni kwa sababu serikali inawajali akinamama.
Alisema tatizo la usafirishaji na usafiri limetatuliwa na biashara zitafanyika kwa wingi zitakazo changia kukuza uchumi wa nchi.
" Kivuko hiki kinabeba wananchi ambao serikali inawathamini sana kuanzia maisha yao pamoja na mali zao hivyo tusingependa masuala mengine kama yaliyotokea yatokee tunamuomba Mungu atuepushe lakini ninachokiona majini ni kivuko ambacho tumelipia billion Sh.4.2kama.kingenunuliwa nje ya nchi kingegharimu Sh. Bilioni 22 lakini kampuni ya ndani ya Songoro Marine ilikubali kukitengeneza kwa gharama ya hizo" anasema Mwakalinga.
Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele akizungumza wakati akizindua kivuko hicho aliwagiza Wakala wa Melinda Nchini TASAC kuhakikisha inaweka maofisa usimamizi katika maeneo yote ya usafiri majini, na kutoa.mafunzo kwa wa wamiliki na waendeshaji wa.vyombo vya majini ikiwamo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
Alisema hatua hiyo itasaidia kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa kuzingatia utaratibu na kanuni zinazosimamia uendeshaji wa vyombo hivyo kuepuka matukio ya ajali.
Aidha, aliagiza TEMESA kusimamishwa kwa ukaribu uendeshaji wa vivuko hivyo ili wananchi wafaidi matunda mazuri ya serikali yao kwa fursa ya maendeleo yao binafsi.
Kamwelwe alisema.kivuko hicho kina ubora kwa kuwa kimewekewa mfumo maalum ambao unaweza.kutambua uzito wa mzigo,abiria pamoja na tarehe ya kufanyiwa matengenezo, huku akitangaza wananchi wa eneo hilo kusafiri bure katika Kivuko jicho kwa siku mbili.
Alisema hataki kuona maafa ya kuzama Kivuko yakitokea tena kama ilivyotokea kwa MV Nyerere kilichozama Ukara miaka miwili iliyopita na kuua mamia ya watu.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kazi kubwa ili aliyoifanya kwani kivuko hicho kimetengenezwa ndani ya miaka miwili hivyo nchi yetu imshukuru Mungu sana kwa kupata kiongozi mahili mwenye maamuzi,maona na anayeguswa na shida za wananachi ambapo ukamilishwaji wa kivuko hicho ni fursa kubwa ya kiuchumi.
" Kupitia kivuko hiki biashara zitazidi kuboreka na vipato vya wananachi vitazidi kuimarika , usafiri ni sekta nyeti kwa maendeleo ya wananchi hivyo amewataka kuitumia meli hiyo kuzalisha ili kupandisha uchumi wao ." alieleza Mongella.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Cornel Magembe alisema alisema tangu ilipotokea ajali ya Mv.Nyerere mwaka 2018 ambapo wananchi walikabiliwa na shida ya usafiri hiyo wanaishukuru serikali kwa kusema na kutenda na kuwaletea kivuko .
"Kwa niaba ya wananchi yake wanatoa shukurani kwa Rais baada ya kutekeleza ahadi yake aliyoitoa baada ya kuielekeza Wizara ya Ujenzi kuunda kivuko kipya ambacho itatatua changamoto ya usafiri katika eneo hili kwani watu walipata tabu sana Sasa wamepata kivuko cha kutumia dakika 40 kutoka Bwisya kwenda Bugolola ambapo awali walitumia masaa mawili" alieleza Magembe.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Japhet Masele alisema, gharama za ujenzi wa kivuko hicho ni Billion 42.2.ambazo zimetolewa na serikali chenye uwezo wa kubeba abiria 300 ,magari 19 na mizigo tani 100.
Alisema Kivuko hicho kimetengenezwa na kampuni ya Songoro Marine iliyopo Jijini Mwanza,kivuko hicho kitawaondolea adha wakazi wa eneo hilo pia ni jukumu la serikali kuwapeleka huduma wananchi pale panapohitajika pia wataendelea kukitunza kivuko hicho .
Kwa upande wake Mjumbe wa Halimshauri Kuu ya CCM, mkoani Mwanza, Jamal Abdul Babu aliwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo Rais John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.