• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Kivuko Cha MV UKARA II Hapa Kazi Tu Chazinduliwa rasmi

Posted on: October 19th, 2020

Serikali imekamilisha ujenzi wa vivuko saba zikiwemo  Ambulance maalum tatu kwa ajili ya kusaidia usafiri katika mikoa mbalimbali hapa nchini vyenye thamani ya Sh. Bilioni 36.36.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano( sekta ya ujenzi) Elias Mwakalinga katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza katika uzinduzi wa Kivuko cha Mv.Ukara II hapa kazi tu.

Alisema  kwa miaka mitano serikalli imejenga vivuko  saba pamoja na Ambulance maalum tatu pia kwa sasa timu ya watalaam wake ipo mkoani kwa ajili ya kufanya utafiti ili kubaini maeneo yanayohitaji vivuko na kuyaainisha.

Pia alisema baada ya ajali  Mv.Nyerere iliyozama September 20 mwaka  2018,ambapo watu takribani 227 walipoteza maisha  serikali kupitia Wizara iliamua kununua kivuko mbadala chenye urefu wa mita 42 na upana wa mita 10 na chumba maalumu cha kujifungulia hiyo ni kwa sababu serikali inawajali akinamama.

Alisema tatizo la usafirishaji na usafiri limetatuliwa na biashara zitafanyika kwa wingi zitakazo changia kukuza uchumi wa nchi.

" Kivuko hiki kinabeba wananchi ambao serikali inawathamini sana kuanzia maisha yao pamoja na mali zao hivyo tusingependa masuala mengine kama yaliyotokea yatokee tunamuomba Mungu atuepushe lakini ninachokiona majini ni kivuko ambacho tumelipia billion Sh.4.2kama.kingenunuliwa nje ya nchi kingegharimu Sh. Bilioni 22 lakini kampuni ya ndani ya Songoro Marine ilikubali kukitengeneza kwa gharama ya hizo" anasema Mwakalinga.

Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele akizungumza wakati akizindua kivuko hicho aliwagiza Wakala wa Melinda Nchini TASAC kuhakikisha inaweka maofisa usimamizi katika maeneo yote ya usafiri majini, na kutoa.mafunzo kwa wa wamiliki na waendeshaji wa.vyombo vya majini ikiwamo Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Alisema hatua hiyo itasaidia  kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa kuzingatia utaratibu na kanuni zinazosimamia uendeshaji  wa vyombo hivyo kuepuka matukio ya ajali.

Aidha, aliagiza TEMESA kusimamishwa kwa ukaribu uendeshaji wa vivuko hivyo ili wananchi wafaidi matunda mazuri ya serikali yao kwa fursa ya maendeleo yao binafsi.

Kamwelwe alisema.kivuko hicho kina ubora kwa kuwa kimewekewa mfumo maalum ambao unaweza.kutambua uzito wa mzigo,abiria pamoja na tarehe ya kufanyiwa matengenezo, huku akitangaza wananchi wa eneo hilo kusafiri bure katika Kivuko jicho kwa siku mbili.

Alisema hataki kuona maafa ya kuzama Kivuko yakitokea tena  kama ilivyotokea kwa MV Nyerere kilichozama Ukara miaka miwili iliyopita na kuua mamia ya watu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kazi kubwa ili aliyoifanya kwani kivuko hicho kimetengenezwa ndani ya miaka miwili hivyo nchi yetu imshukuru Mungu sana kwa kupata kiongozi mahili mwenye maamuzi,maona na anayeguswa na shida za wananachi ambapo ukamilishwaji wa kivuko hicho ni fursa kubwa ya kiuchumi.

" Kupitia kivuko hiki biashara zitazidi kuboreka na vipato vya wananachi vitazidi kuimarika , usafiri ni sekta nyeti kwa maendeleo ya wananchi hivyo amewataka kuitumia meli hiyo kuzalisha ili kupandisha uchumi wao ." alieleza Mongella.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Cornel Magembe alisema alisema tangu ilipotokea ajali ya Mv.Nyerere mwaka 2018 ambapo wananchi walikabiliwa na shida ya usafiri hiyo wanaishukuru serikali kwa kusema na kutenda na kuwaletea kivuko .

"Kwa niaba ya wananchi yake wanatoa  shukurani kwa Rais  baada ya kutekeleza ahadi yake aliyoitoa baada ya kuielekeza Wizara ya Ujenzi kuunda kivuko kipya  ambacho itatatua changamoto ya usafiri katika eneo hili kwani watu walipata tabu sana Sasa wamepata kivuko cha kutumia dakika 40 kutoka Bwisya kwenda Bugolola ambapo awali walitumia masaa mawili" alieleza Magembe.  

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Japhet Masele alisema, gharama za ujenzi wa kivuko hicho ni Billion 42.2.ambazo zimetolewa na serikali chenye uwezo wa kubeba abiria 300 ,magari 19 na mizigo tani 100.

Alisema Kivuko hicho  kimetengenezwa  na kampuni ya Songoro Marine iliyopo Jijini Mwanza,kivuko hicho kitawaondolea adha wakazi wa eneo hilo pia ni jukumu la serikali kuwapeleka huduma wananchi pale panapohitajika pia wataendelea kukitunza kivuko hicho .

Kwa upande wake Mjumbe wa Halimshauri Kuu ya CCM, mkoani Mwanza, Jamal Abdul Babu aliwaomba wananchi hao kumpa kura za ndiyo Rais John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu ujao.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.