LENGO LILILOKUSUDIWA NANE NANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI LIMEFANIKIWA:RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza kamati ya maandalizi ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima (Nane nane) 2024 kwa maandalizi ambayo yamefanyika katika viwanja vya Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Mhe. Mtanda ametoa pongezi hizo leo Agosti 08, 2024 wakati alipokuwa akihutubia wananchi waliojitokeza katika kilele cha sherehe za Nane nane Kanda ya Ziwa Magharibi (Mwanza, Geita na Kagera), Mhe. Mtanda amesema amefanikiwa kupita katika mabanda mbalimbali ya waoneshaji ameona na kujifunza teknolojia mbalimbali hakika lengo lililokusudiwa limefanikiwa.
"Nimefurahi kuona baadhi ya bidhaa na huduma zinazopatikana katika maonesho haya, nimetembelea makampuni, Taasisi, huduma za kifedha za mikopo ya kilimo, Taaisisi za elimu na zile za utafiti mkusanyo wa wadau wote hawa umechangia hamasa kubwa kwa wananchi wetu wa kanda ya ziwa nawapongeza na kuwahukuru sana". Mhe. Mtanda.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesena katika maonesho hayo Wakulima na wananchi kwa ujumla pia wamepata nafasi ya kuona, kujifunza na kubadilishana uzoefu, teknolojia juu ya bidhaa na huduma mbalimbali na hivyo kupanua wigo wa uelewa kuhusu uzalishaji, uongezaji thamani wa mazao pamoja na mtandao wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa.
"Maonesho haya pia yametumika kuonesha mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ndivyo ambavyo watu wengi wetu tunatarajia kuona mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye sekta hizi za kiuchimi". RC Mtanda.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa pia ametumia wasaa huo kuwakumbusha na kuwaomba wananchi kushiriki zoezi muhimu kwa Taifa la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa amani, nidhamu na utulivu ili tuilinde amani ya nchi.
Akuzungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella ameipongeza pia kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo huku akisema amekuwa akihudhuria maonesho hayo kwa kipindi cha miaka miwili lakini sherehe za mwaka huu zimefana sana.
Maonesho na sherehe za Wakulima kwa mwaka 2024 yamefanyika kwa kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.