• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MAAFISA ARDHI ILEMELA MATATANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Posted on: July 16th, 2024

MAAFISA ARDHI ILEMELA MATATANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani humo kuwakamata Mkuu wa Idara ya Ardhi wa Manispaa ya Ilemela Grace Masawe pamoja na Afisa Mipango Miji Mwajuma Mabula kwa tuhuma za kuomba Rushwa.

Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo leo  Julai 16, 2024 mtaa wa Igoma kwenye mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi na ndugu Matiko Migire kuwasilisha kero kwamba watumishi hao wamemuomba rushwa ya Tshs. 2,430,000 ili wafanye upimaji wa viwanja na. 311, 312 na 313 Block A Pasiansi.

Mhe. Mtanda amesema kitendo hicho si cha kiungwana na kinawanyima haki wananchi  hivyo wakati TAKUKURU wanalichunguza suala hilo idara ya ardhi amewapa siku saba kukamilisha upimaji wa viwanja hivyo kwani wamemzungusha kwa muda mrefu mteja huyo anayefuatilia bila mafanikio.

Awali, akiwasilisha kero hiyo kwa Mkuu wa Mkoa, Matiko alifafanua kuwa mwaka 2019 Halmashauri hiyo iliomba Hati za viwanja hivyo na kuzifuta na kuahidi kufanya upimaji mwingine na kuwataka wamiliki Joseph Mashiku, Hezeline Chawachi na Desderius Ntobi kwa gharama ya 500,000 ambayo wametoa namba ya kulipia.

Ameendelea kusema kwamba idara hiyo ya ardhi haijawahi kutekeleza ahadi yao kwenye viwanja hivyo na badala yake wamekua wakimtafuta kwa simu kupitia mtuhumiwa Mwajuma na kumtaka atume kiasi hicho (2,430,000) ikiwa fedha halali anayotakiwa kulipia huduma ni Tshs. 500,000 tu.

Akizungumzia kero ya maji kwenye baadhi ya mitaa ya Nyamagana, Mhe. Mtanda amesema kupitia mkopo wenye masharti nafuu wa Tshs. Bilioni 400 kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) Mamlaka ya Maji (MWAUWASA) itasambaza maji kwenye umbali wa zaidi ya Kilomita 700 kutoka chanzo cha Butimba na watamaliza kero kwa wananchi wengi.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.