• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Maafisa Ushirika Kanda ya ziwa wajengewa Uwezo Mwanza

Posted on: November 22nd, 2021

Maafisa Ushirika Kanda ya Ziwa na Kigoma wamejengewa uwezo wa ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika ili kuweza kuwa na udhibiti mzuri wa vyama hivyo huku wakitakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwakuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazosimamia majukumu yao.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ameeleza kuwa Serikali haitomfumbia macho Afisa Ushirika yeyote au Mtendaji yeyote wa Serikali atakayebainika kuvihujumu Vyama vya Ushirikka kwa namna yeyote ile.

Anasema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuiendeleza sekta ya Kilimo kwa lengo la kumsaidia mkulima mmoja mmoja kwani  kilimo kitakuwa na manufaa makubwa endapo mazao yanayozalishwa  yana soko la uhakika na wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati.

Anasema Ili kufanikisha azma hiyo, serikali imeendelea kuhamasisha Wananchi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujiunga au kuanzisha vyama vya Ushirika katika maeneo yao ambapo serikali itaendelea kuvisimamia vyama hivyo  ili viweze kuwasaidiawakulima katika kuzalisha na kuuza mazao yao, kuwalipa fedha kwa wakati na kusaidia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati.

Anaeleza kuwa taarifa za ukaguzi unaofanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) zimekuwa zikionesha madhaifu makubwa kila mwaka ambao wakati mwingine ni kutokana na usimamizi usioridhishawa Maafisa Ushirika ambao ndio wasimisizi wa karibu sana wa vyama hivyo.

"Pamoja na jitihada za Serikali katika kuendeleza kilimo chenye manufaa kwa wakulima na kusimamia vyama vya Ushirika ili viwasaidie wakulima bado kumekuwepo changamoto nyingi kwenye yama hivyo nyingi  zinatokana na usimamizi usioridhisha  hivyokupelekea mianya ya madhaifu mbalimbali hususan upotevu wa fedha na mali zingine za wanaushirika "Mkuu wa Mkoa  anaeleza na kuongeza kuwa,

"Udhibiti na usimamizi katika vyama hivyo umekuwa mdogo kutokana na hawa ambao ndio wenye jukumu la kuvisimamia vyama hivyo  katika maeneo yao kwa kila Wilaya kukosa ujuzi na uzoefu wa kusimamia kwa  weledi unaotakiwa, mfano; vyama vya ushirika vinatakiwa kukaguliwa lakini vimekuwa havikaguliwi kikamilifu kutokana na Maafisa kukosa ujuzi wa ukaguzi, ujuzi huu unakosekana kwa sababu ya ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara kwa Maafisa hao hivyo mafunzo haya yajikite katika kutatua changamoto za kiujuzi na kiutendaji kwa Maafisa." anaeleza.

Anasema uwepo wa malalamiko mengi

 kutoka kwa wakulima juu ya baadhi ya

Maafisa Ushirika kukiuka taratibu za utumishi wa Umma na kujiingiza katika

vitendo vya rushwa, usababishaji wa migogoro na kushirikiana na baadhi ya

watendaji wa Vyama vya Ushirika katika kuvihujumu Vyama hivyo anafurahi kusikia  hatua za nidhamu zimekuwa zikichukuliwa kwa wote waliothibitika kufanya matendo hayo.

Kwa upande wake Dkt .Benson Ndiege ,Mrajis wa vyama vya ushirika na Mtendaji anaeleza  tume ya maendeleo ya ushirika ni taasisi iliyopewa dhamana  ya kusimamia maendeleo ya ushirika nchini na inasimamia sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 namba 6 .

Anasema sheria inataja majukumu mawili ambayo ni uhamashishaji wa ushirika na udhibitisho ama usimamizi wa vyama vya ushirika ambapo katika eneo ambalo lina tatizo ni Udhibiti na usimamizi ambalo linahitaji uangalizi kwani utafiti walioufanya unaonyesha vyama vingi vya ushirika mwaka 2019 na 2020 asilimia 60 ndivyo vimeweza kukaguliwa na kusimamiwa ipasavyo vingine vyote asilimia 40 havikuweza kufikiwa ipasavyo.

" Tulijiuliza ni kwa nini ili lilitokea Utafiti wetu unaonyesha kuwa labda changamoto ipo kwa maafisa ushirika kwa sababu takwimu zinaonyesha asilimia zinaonyesha asilimia 33 ya maafisa hao ndio wenye uwezo wa kukagua kikamilifu vyama vya ushirika vya aina mbalimbali ili uweze kutoka kwenye hili dibwi lazima asilimia 100 ya maafisa ushirika wawe na huo uwezo hapo ndipo wataondokana na hilo tatizo la kutokagua vyama vya ushirika na kutovisimamia ipasavyo ."anaeleza

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ,Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara anasema unatambua umuhimu wa mafunzo hayo imani yao mafundisho waliyoyapata wataenda kufanya vizuri.

Alisema kuna mambo makubwa yanayofanyika mkoani humo  ikiwemo ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ambalo limeanza kwa kasi kubwa hivyo tuendelee kuhamasisha vyama vya ushirika ili viweze kujiunga katika shughuli hiyo hadi sasa wanavyama 21 ambavyo vimejiunga na vimeomba mkopo wa billion 3.2 .

Hivyo aliwaomba na Maafisa ushirika ndani na nje ya Mkoa wanaoishi maeneo ya ziwa waweze kuhamasisha ufugaji huo .

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI MWANZA

    May 10, 2025
  • SERIKALI KUNUNUA MTAMBO RASMI WA KUSAFISHA ZIWA VICTORIA

    May 10, 2025
  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.