MADAKTARI BINGWA WA RAIS DKT. SAMIA KUWEKA KAMBI YA SIKU 5 MWANZA
Madaktari Bingwa wa Rais Mhe. Dkt. Samia wamewasili katika Mkoa wa Mwanza leo Juni 17 2024, ambapo watatoa huduma za kibingwa kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kwenye Halmashauri zote mkoani humo.
Huduma hizo zikiwemo upasuaji mkubwa wa magonjwa ya wakina mama,Figo na Saratani zitatolewa kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 17 - 21 mwaka huu
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha na kuwapokea madaktari hao, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana amesema anawashukuru madaktari hao wapatao 45 na ameishukuru Wizara ya Afya kwa kufanikisha jambo hilo muhimu ambapo wananchi watapata huduma za kibingwa kwa gharama ndogo.
"Huduma zitawafikia wanachi huko waliko kwa gharama ndogo lakini mgonjwa atatakiwa kuchangia kiasi kidogo iwapo atahitajika kupata huduma zinginezo ikiwemo huduma ya vipimo, dawa na huduma za upasuaji",amesema Mtendaji huyo wa Mkoa
Aidha Balandya ametoa wito kwa wananchi wote wenye matatizo ya kiafya kuhudhuria kwenye hospitali hizo za Wilaya kuonana na kutibiwa na madaktari bingwa ambapo itawasaidia kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu nje ya Wilaya zao kufuata huduma.
Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Bi. Fideo Obimbo amesema lengo la ujio wa madaktari hao bingwa ni kuwafuata wagonjwa wale ambao hawana uwezo wa kufikia huduma za kibingwa na kampeni hiyo imelenga kufikia mikoa yote 26 ambapo kwa sasa wamefikia mikoa 20.
"Kampeni hii imekuwa na matokea chanya ambapo mpaka sasa tumeshafikia wagonjwa 51471, miongoni mwao wagonjwa 6571 tuliweza kuwapatia huduma na wakalazwa katika hospitali hizo hizo za ngazi za chini",Fideo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.