• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Maji Sengerema Asilimia kwa 100%

Posted on: July 5th, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka wananchi wa Sengerema na mkoa wa Mwanza kwa ujumla kulinda na kutunza ziwa Victoria kwa kukomesha uvuvi haramu katika ziwa hilo.

Rais ameyasema hayo wakati akizindua mradi mkubwa wa maji na usafi wa Mazingira uliogharimu fedha za kitanzania zipatazo Bil. 22.4 Wilayani Sengerema mkoani hapa.

Mh. Rais, amesema nilazima suala la uvuvi haramu likemewe kwa nguvu zote na kwa ngazi zote, “Nimeambiwa wapo baadhi ya watu kwa kushirikiana na watumishi wa umma wasio wa aminifu wanaendesha uvuvi haramu, nitoe wito kwa yeyote atakaye bainika kufanya hivyo, serikali haitakuwa na msamaha kwake” alisema Mh. Rais.

Rais Magufuli aliesema, mtu anapotumia sumu ziwani anauwa hata viumbe visivyo husika na zaidi sana dawa zinazotumika kusafisha maji hazina uwezo wakuondoa kemikali, hivyo nilazima kila mwananchi aelewe kutumia sumu ya thiodani ziwani ni hatari kwa maisha yao".

Ameongeza kuwa, kukamilika kwa mradi huo ni kukamilisha ahadi aliyo ahidi katika kampeni zake za mwaka 2015 wakati akiomba kura ambapo, kwa sasa wananchi wa Sengerema watapata maji kwa asilimia 100.

Kwa upande wake, Waziri maji Mhandisi Gerson Lwenge, amesema mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 15.84 na kunufaisha wakaazi wapatao 138,000 wa mji wa Sengerema na vijiji vya jiarani vya Nyamazugo, Kijuka, Mwaliga na Nyamizeze kwa asilimia 100 hadi kufikia mwaka 2030.

Awali akitoa salaam za Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema mkoa huo kwa sasa umejipanga kikamilifu kwenye mageuzi ya Mapinduzi ya viwanda, huku akimhakikishia Mh. Rais uwepo wa Viwanda 12 vikubwa ambavyo vipo tayari kwakufunguliwa.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema, mkoa umeamua kuweka nguvu kubwa katika zao la Pamba, ‘Mh. Rais katika Msimu wa 2016/2017 mavuno yetu ya Pamba yalifikia tani Mil.5, lakini katika msimu huu, tunatazamia kupata sio chini ya tani Mil. 20.

Naye Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, akishukuru kwa niaba ya wananchi wa Sengerema alisema, wanamshukuru sana Mh. Rais kwakuendelea kuwatumikia watanzania kwa moyo wa uaminifu lakini zaidi sana kukamilisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo inayo himiza kuwa na maji safi na salama kwa Vijijini kwa asilimia 85 na mijini asilimia 95,

“Mh. Rais yawezekana ni kweli wananchi wa Sengerema waliteseka kwa muda mrefu, lakini sisi wanasiasa yawezekana tulikuwa na shida kubwa zaidi, maana mradi huu umekuwa wa muda mrefu na mahali pengine hata tulipokuwa tukiongea majukwaani  walikuwa hawatuelewi ”alisema Ngeleja.

Kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa maji katika Mji wa Sengerema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ni ishara kwamba Mji wa Sengerema sasa utapata maji kwa asilimia miamoja ambapo wananchi wapatao 138,000 watanufaika na mradi huo.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • LENGO LA HOSPITALI ZA WILAYA NI KILA MWANANCHI APATE HUDUMA MAHALI ALIPO - WAZIRI MKUU

    May 19, 2025
  • MITAMBO YA KUOPOA MAGUGUMAJI KUWASILI MWISHONI MWA MWEZI JULAI.

    May 19, 2025
  • WAZIRI MKUU AWATAKA WANAMALYA KUCHANGAMKIA FURSA YA CHUO CHA MICHEZO

    May 18, 2025
  • NIA YA SERIKALI KILA MWANANCHI AUNGANISHIWE MAJI NYUMBANI KWAKE - WAZIRI MKUU

    May 18, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.