• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MAMILIONI YA RC MAKALLA KWA PAMBA JIJI FC KUANZA KUMWAGIKA LEO

Posted on: March 30th, 2024

MAMILIONI YA RC MAKALLA KWA PAMBA JIJI FC KUANZA KUMWAGIKA LEO


*RC Makalla ahimiza ushindi mfululizo mechi 4 zilizobaki


*Pamba Jiji kuvuna mapesa dhidi ya Maafande wa Polisi Tanzania


*Mashabiki watakiwa kuujaza uwanja wa Nyamagana kuwapa ari Pamba Jiji


Timu ya soka ya Pamba Jiji FC leo Machi 30,2024 inatupa karata nyingine muhimu katika michuano ya ligi ya Championship kwa kuwakaribisha Maafande wa Polisi Tanzania na kuanza safari ya kuoga mapesa ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.CPA.Amos Makalla kwa kila goli kununuliwa kwa shs milioni moja.

Mapema wiki hii Makalla ambaye ni mlezi wa timu hiyo kipenzi cha wana Mwanza inayoshikilia nafasi ya pili na mtaji wa alama 55, aliwatembelea mazoezini uwanjani Nyamagana na kuwapa mikakati yote ya ushindi na kuwatahadharisha kuepukana na njama zozote chafu zitakazo fanywa na wapinzani wao kwa michezo yao iliyosalia.

Mkuu huyo wa mkoa katika mazungumzo hayo aliwaongezea hamasa wachezaji wa Pamba Jiji kwa kuwatangazia kununua kila goli shs milioni 1 michezo yao minne iliyosalia kauli iliyopokelewa kwa shangwe na wachezaji hao.

"Mmenifurahisha sana na matokeo ya michezo yenu iliyopita na  sasa tupo nafasi nzuri na nimeruhusu bonasi itolewe ya shs milioni 5.2,ila msibweteke kazeni buti ongezeni kiwango dimbani kila mechi mbele yetu iwe kama fainali,"amehimiza mlezi huyo.

Amebainisha timu zinazonyemelea nafasi za kufuzu kucheza ligi kuu msimu ujao hazipishani sana alama na Pamba Jiji hivyo kinachotakiwa sasa ni kuhakikisha wanashinda ili kuzidi kuwatimulia vumbi wapinzani wao.

Nahodha wa timu hiyo na mchezaji mkongwe Jerryson Tegete amemuhakikishia mlezi wao kuwa wamejipanga vizuri kwa michezo yao iliyosalia kwani tayari taa ya endiketa ya kucheza ligi kuu wameshawasha hivyo wana Mwanza wazidi kuwaunga mkono.

Baada ya mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya Polisi Tanzania inayoshikilia nafasi ya 8 yenye alama 35, Pamba Jiji FC maarufu kama TP Lindanda wataendelea kusalia dimba lao la nyumbani ambapo Aprili 14,2024 watamenyana na timu ya FJ Talent kutoka Ruvuma kabla ya kuwafungia safari Arusha timu ya TMA mchezo utakaopigwa Aprili 28,2024

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.