Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameongoza kikao cha Ushauri cha Mkoa kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kujumuisha wajumbe mbalimbali wa kikao hicho ikiwa ni pamoja na Mhe.Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt.Charles,Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula, Waheshimiwa Wabunge,Wakuu wa Wilaya,wakurugenzi,Meya wenyeviti na baadhi ya walikwa kutoka Taasisi mbalimbali.
Mhe. Mongella pamoja na kutoa Maagizo mbalimbali kwa watendaji kuhusiana na hoja zilizojitokeza kutoka kwa wajumbe wa Kikao hicho ,alisisitiza kuhusiana na Makusanyo ya Mapato ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na Matumizi ya Mfumo wa Kieletroniki (LGRCIS),’’Halmashauri yoyote isiyotumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya ndani inakiuka taratibu na sheria na ikibainika itachukuliwa hatua za kisheria ”.
Akiwasilisha Taarifa ya Makusanyo ya Mapato ya Ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa Afisa Usimamizi Fedha wa Mkoa Charles Julius Misango ameeleza kuwa Halmashauri za Mkoa wa Mwanza zilijiwekea malengo ya kukusanya jumla ya TZS 35,552,216,000.00 na Jumla ya TZS 9,812,583,537.17 sawa na 28% ya lengo zimekusanywa kwa kipindi cha Julai hadi Novemba, 2017 ambapo kwa kipindi cha Julai-Novemba cha Mwaka 2017/2018 makusanyo halisi ya Mapato ya Ndani yameongezeka kwa asilimia 3.2 (9,812,583,537.17 kutoka 9,507,901,255.23) ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Julai–Novemba cha mwaka wa fedha uliopita 2016/2017.
Misango ameongeza kuwa,ongezeko hili la 3.2% si haba, hasa ukizingatia uchukuliwaji wa vyanzo vikubwa vya mapato kama vile kodi za majengo, Bill boards kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa na kwenda Serikali Kuu (TRA),pia Mfumuko wa bei umedhibitiwa na umeendelea kubakia katika wigo wa tarakimu moja (Current Inflation rate is 5% as per August,2017).
Aidha, Mfumo wa kieletroniki wa Makusanyo ya Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (local Government Revenue Collection System-LGRCIS), ulianzishwa na unasisitizwa utumike kwasababu kuu ya kuwezesha ukusanyaji wa Mapato na taarifa kwa vyanzo vyote mapato vinavyopaswa kukusanywa kisheria na Mamlaka za Serikali za Mitaa,kuhifadhi kumbukumbu za walipa kodi na kutoa hati za madai (ankara) stakabadhi (risiti) kwa walipa kodi, ushuru na tozo mbalimbali kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa,kusimamia Ukusanyaji wa Mapato kwa urahisi zaidi na Utunzaji wa Kumbukumbu za walipa kodi kwa maana ya watu, wafanyabiashara wadogowadogo na makampuni.
Hata hivyo,Mfumo wa mapato unasaidia kufanya usuluhishi wa taarifa za mapato ya fedha zilizokusanywa.Makusanyo yaliyokusanywa kwa mwaka husika yanasidia sana katika kufanya tathmini na kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka Makadirio sahihi na Malengo katika Mipango yao kwa miaka inayofuata ikiwa ni pamoja na kurahisisha Uhakiki na Ukaguzi wa fedha za Umma kwani unazuia udanganyifu unaoweza kujitokeza kwa watumishi wasio waaminifu.Mfumo huu wa ukusanyaji wa mapato (LGRCIS) unasaidia upatikanaji wa taarifa na ripoti mbalimbali kwa haraka na pindi tu zinapohitajika ikiwa ni pamoja na kuongeza dirisha la upatikanaji wa taarifa kwa ngazi ya Taifa na kutoa taarifa za kina za vyanzo vya mapato,kudhibiti Mianya ya rushwa na mapato ya Halmashauri na pia Kutumika kama chanzo cha Mipango na Bajeti za Maendeleo kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa pia malipo kwa njia ya kieletroniki yameongeza uwazi na usalama wa fedha zinazokusanywa na Mfumo huu wa Mapato (LGRCIS).
Misango ameongeza kuwa, Mfumo huu unarahisisha na kuongeza wigo wa ulipaji kodi kwa wananchi kwa kuwezesha njia mbalimbali za kieletroniki za ulipaji wa miamala ya kifedha, ikiwa ni pamoja na kupitia mifumo mbalimbali ya kibenki na huduma za kifedha za makampuni ya simu za kiganjani pia Mlipa kodi kutumia muda mwingi kwenye uzalishaji na kutumia muda mfupi katika ulipaji na kupewa stakabadhi yake papo hapo bila tena kuhitajika kurudi kwa mlipaji (cashier) wa Halmashauri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.