• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mhe.Majaliwa aahidi makubwa Wilaya ya Magu

Posted on: September 22nd, 2020

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa amewaahidi wananchi wa Wilaya ya Magu vituo vya afya, maji, barabara na umeme na kuwataka kuchagua viongozi makini watakaoleta maendeleo.

Ametoa ahadi hiyo  kwa wananchi wa Kijiji cha Kisamba Kata ya Lubugu na Irungu Kata ya Nyigogo wilayani Magu akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza akitokea mkoani Mara.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo makubwa ya kuhudumia jamii na kuleta maendeleo chini ya Rais Mhe.John Magufuli, hivyo waichague tena CCM kwa miaka mingine mitano kwa sababu ina uwezo wa kuratibu mambo yote na inatambua changamoto za wananchi wake.

“Mhe.Rais Dkt. Magufuli amefanya makubwa ya kuhudumia jamii katika sekta za afya,elimu, maji na barabara kazi ambayo ni ya miaka mitano na tutaifanya tena, kwa sababu sera yetu ni maendeleo  mpeni miaka mitano migine afanye maendeleo makubwa ya nchi hii,”alisema Mhe. Majaliwa.

Ameongeza kuwa Magu bado kuna changamoto ya vituo vya afya, serikali  itajenga vingine ingawa imekamilisha vituo vya afya Kahangara (sh. bilioni 1.4), Lugeye (sh. milioni 400) na Kabila (sh.milioni 400) ambapo kituo cha Kahangara kitaongezewa sh. milioni 400, pia itatoa sh. milioni 200 za upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Magu.

“Tumejenga vituo vya afya vya kimkakati vyote vina huduma zote ambapo kutokana na mahitaji ya dawa kuongezeka tumetoa sh. bilioni 10.8 ili kuwezesha upatikanaji wa dawa ili wananchi wasiendelee kununua kwenye maduka binafsi,”alisema Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM  na kusisitiza;

“Huduma za matibabu ni bure kwa wazee, watoto chini ya miaka mitano na huduma ya kujifungua kwa akina mama wajawazito, kama kuna watendaji wanakwamisha wanawatoza fedha hao ni wauaji, kama fedha zipo kwa nini uwatoze fedha,  twambieni wachukuliwe hatua.”

Mhe. Waziri Mkuu pia alisema serikali iko kwenye mchakato wa kutekeleza muswada wa Bima ya Afya kwa Watanzania wote wapate matibabu na itatoa magari ya kubeba wagonjwa mahututi  na wa dharura hasa wajawazito kwenye vituo vyote vya afya nchini vikiwemo vya Wilaya ya Magu.

Aidha alisema endapo wananchi wa Magu wataichagua CCM  mkakati wa serikali ni kuhakikisha wilaya hiyo inapata maji ya uhakika na tayari imepeleka shilingi bilioni 23 .3 za miradi ya majina kufafanua kuwa mradi wa maji kwenye vijiji vya  Kinango (Sh.milioni 107),Matela (sh.milioni 397),Kabale (sh.milioni 231),Buhumbi, Bugatu, Ndagalu, Nyasato (sh. bilioni 2.1) na Nsolo (sh.Bilioni 1).

Pamoja na hayo pia aliahidi  kujenga miundombinu ya barabara za makao makuu ya wilaya kwa  kiwango cha lami ambapo kwa Magu imetenga mabilioni ya fedha za ujenzi wa barabara za Bujora, Magu-Ngudu, Shishani hadi Simiyu.

“Umeme bado kwenye vitongoji na mitaa, vyote vitapata na utafungwa hata kwenye nyumba za tembe kwa sh. 27,000, nguzo  bure hadi nyumbani. Kwenye kilimo cha pamba tunataka kujenga viwanda vya kuchambua pamba tuingie kwenye na kuzalisha nyuzi,”alisema Mhe. Majaliwa.

Aliongeza kuwa serikali imefanya kazi kubwa kwa miaka mitano na kwenye uchaguzi wa mwaka huu anatafutwa kiongozi makini mwenye uwezo wa kusimamia serikali yake na kuwaunganisha watanzania.

Mhe.Majaliwa amedai anatakiwa kiongozi wa kukomesha rushwa inayoathiri  maendeleo atakayeweza kuwahudumia wanyonge na kusimamia rasilimali za nchi ziwanufaishe wananchi wote.

" Tunayo sababu ya kumpigia kura Mhe.Rais Dkt.Magufuli, amefanya kazi kubwa, maendeleo hayana chama ndo maana nimekuja kumwombea kura  ameongoza nchi yenye watu zaidi ya milioni 60 yenye makabila mengi na wenye itikadi ya vyama tofauti,hivyo tumpe tena miaka mingine mitano ili afanye maendeleo mengine zaidi," alisema Mhe. Majaliwa.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga alisema  wananchi wa Magu kwa miaka mitano wamepata mafanikio mengi hivyo wana haki ya kumpa kura Mhe.Rais Magufuli Oktoba 28, mwaka huu.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.