Mkuu wa Wilaya ya Misungwi atakiwa kuongeza nguvu, kukamilisha na kufanya vitu vya tofauti katika mradi wa ujenzi wa hospital ya Wilaya hiyo ulioanza June mwaka huu.
Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella alisema kazi ni zuri lakini waongeze nguvu kwani fedha hizo za Force Account zinatumika ndani ya siku 90 na ujenzi uwe umekamilika .
" Huko nyuma yalifanyika mauzauza na wengine tulishiriki Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi tufikiri tofauti kuongeza kasi na kufanya vitu vya tofauti ili kuwatofautisha na wengine ambavyo vitakuwa kumbukumbu ata mtu akiona anasema fulani alifanya hiki chamsingi tuwe waadilifu na tupige kazi na kukaza buti na tufanye vitu vya tofauti " alieleza Mongella.
Pia aliwaomba wananchi kuendelea kuvilinda vifaa vinavyotumika katika ujenzi sambamba na kufanyia kazi huku akisiaitiza fedha hizo za ujenzi zimetolewa na Mhe.Rais Magufuli.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Zabron Masatu anasema fedha iliyopokelewa katika awamu ya kwanza Million 500 (500,000,000) imeelekezwa kujenga majengo matatu ambayo ni jengo la OPD, jengo la maabara na kichomea taka.
"Hospital hii ikikamilika itahudumia wananchi wa eneo hili wapatao 462,855 ,pia uongozi wa Wilaya kwa niaba ya wananchi tunatoa shukrani nyingi kwa serikali hii inayoongozwa na Raise wetu Mhe Dkt. John Magufuli kwa kuwezesha ujenzi wa kihistoria wa hospitali ya wilaya,tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana nasi katika kuleta maendeleo ya jamii kuelekea uchumi wa kati." anasema Masatu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.