Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally akiwa safarini kuelekea Mkoani Shinyanga mapema leo Machi 15, 2023 amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na kufanya mazungumzo mafupi.
Shikh Zuber amesema pamoja na mambo mengine kwenye ziara yake kama ukaguzi wa Miradi iliyo chini ya Baraza la Waislam nchini, anakemea vikali Uovu kama mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo limeonekana kutaka kuharibu nguvukazi ya Taifa.
Vilevile, amesema Taifa linaweka nguvu sana kwenye kuimarisha amani hivyo ametoa wito kwa Kamati za amani katika kila ngazi kuendelea kuhimiza masuala ya amani wakati wote ili kuikumbusha jamii umuhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Aidha Shekhe Mkuu amewataka Waislamu nchini kujiandaa na Mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufunga na kufuturisha pamoja na kutenda matendo mema yanayomfurahisha Mwenyezi Mungu.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amemshukuru Shekhe Mkuu amemuahidi ushirikiano na amebainisha kuwa Serikali ya Mkoa huo imeweka nguvu kwenye kukomesha Matendo Maovu hususani Ukatili kwa watoto na kwamba tayari kuna mkakati wa makusudi wa kutoa Elimu kwenye taasisi za Elimu mkoani humo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.