MWENGE WA UHURU KUKIMBIZWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO MISUNGWI LEO
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Mapema leo tarehe 18 Julai, 2023 imepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea wilayani Sengerema tayari kwa kuukimbiza kwenye miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 995.
Akizungumza kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye kivuko cha Kigongo, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Paul Chacha amebainisha kuwa wamejiandaa vema kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kufika kwenye miradi iliyotekelezwa kwa ubora mkubwa.
Mhe. Chacha amefafanua kuwa, uwapo wilayani humo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye miradi iliyotawanyika eneo la umbali wa KM 90.7 na kwamba wana shauku kubwa ya kuukimbiza ili uangaze miradi iliyotekelezwa vizuri.
"Mwenge wa Uhuru utapokuwa kwenye Wilaya yetu leo utaweka mawe ya msingi kwenye miradi miwili, kufunguliwa mmoja, mradi mmoja utakaguliwa pamoja na mmoja utakaozinduliwa na miradi hiyo ipo kwenye sekta za Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii." amefafanua Mhe. Chacha
Naye, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameomba ushirikiano kwa Halmashauri hiyo na amewataka kuwa wazalendo kuipinga rushwa kwa vitendo ili kuunga juhudi za Mhe. Rais za kuleta maendeleo nchini.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 inasema "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.