RAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI BUTIMBA, ALETA KICHEKO KWA WANA MWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo juni 20, 2025 amezindua mradi wa Maji na chanzo cha kutibu na kusafisha maji uliojengwa na Kampuni ya Sogea Satom na Vinci Grand Projects kutoka Ufaransa kwa thamani ya zaidi ya Tshs. Bilioni 70.
Akizungumza na wananchi katika hafla ya iliyofanyika katika viwanja vya mradi huo Butimba jijini Mwanza Mhe. Rais amesema mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 48 kwa siku utasaidia kuongeza mtandao wa usambazaji maji ndani na maeneo ya pembeni mwa jiji hilo takribani watu 450,000.
Aidha, amewapongeza MWAUWASA kwa usimamizi na amewashukuru wadau wa maendeleo waliotoa ruzuku na mikopo pamoja na Mkandarasi kwa ujenzi wa mradi huo na akawataka wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na baadaye.
Ameongeza kuwa miradi ya maji na usafi wa mazingira inayotekelezwa kila kona nchini imedhamiria kutegua kitendawili cha upatikanaji wa maji safi na salama na akawasihi wananchi kujenga uchumi wao kwa uvuvi na kilimo lakini wahakikishe wanahifadhi mazingira na vyanzo vya maji.
Naye, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amebainisha kuwa awali mkoani wa Mwanza ulikua na chanzo kimoja tu kikubwa cha maji cha Capripoint ambacho kinazalisha lita milioni 90 kwa siku na kwamba kutokana na ongezeko la watu chanzo hicho kimekua finyu na ndipo serikali ikaamua kujenga chanzo kipya.
“Mhe. Rais, ilikuwa ni kitendawili kikubwa, wana mwanza wa Nyamagana na Ilemela walikuwa wanahoji kwanini ziwa lipo mwanza na wao wanakosa maji”, amesema Mhe. Aweso.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Said Mtanda amesema mahitaji ya maji kwa sasa ni lita milioni 172 kwa siku huku vyanzo vya Capripoint na Butimba vikizalisha lita 138 na kwamba vimesaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji Maji kutoka 59% (2021) hadi 85% (2025) sawa na ongezeko la asilimia 25.
Aidha, amefafanua kuwa sekta ya maji Mkoani Mwanza imeimarika sana kwani kwa vijijini kupitia Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wametekeleza miradi zaidi ya 180 yenye thamani ya zaidi Bolioni 100.3 na hali ya upatikanaji imeongezeka hadi zaidi ya asilimia 78.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.