• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS Mwanza afanya ziara ya ukaguzi wa Huduma Sekta ya Afya Wilaya za Mwanza na kutoa maagizo

Posted on: May 12th, 2022

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Afya na Vifaa Tiba katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema na Misungwi Mkoani Mwanza na kutoa maelekezo ya marekebisho ya haraka.


Akiwa Halmashauri ya Buchosa Katibu Tawala Samike ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Buchosa kuhakikisha Vituo vyote vya Afya vilivyokamilika kuanza kutoa huduma haraka ili kuwapunguzia kutembea umbali mrefu Wananchi.


Aidha ametoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Irene Mukere kuhakikisha Vituo vyote vya Afya vinatumia mfumo sahihi wa Serikali wa ukusanyaji malipo.



"Tusiombe dawa nyingi kutoka Bohari Kuu ya Serikali tofauti na mahitaji, hali hii inasababisha hasara kutokana na dawa kukaa muda mrefu na kuchina"



Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa,Julius Mlongo amesema baada ya ziara hiyo ya Katibu Tawala Mkoa sasa ni jukumu letu kuzifanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika Miradi ya Serikali ili kuwaletea Maendeleo Wananchi.


Akiwa Wilayani Misungwi katika ziara yake ya ukaguzi wa Huduma za Afya,Vifaa Tiba na utendaji kazi,Katibu Tawala Ngusa Samike ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kujenga Hospitali,Vituo vya Afya na Zahanati kwa haraka na usahihi mzuri wa gharama.


Aidha ametoa maagizo ya kutumiwa kila mwezi taarifa ya Maendeleo ya miradi ya Afya na ili kuona mabadiliko chanya ya ziara yake.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Benson Mihayo amesema wamejipanga  kuhakikisha fedha zote zilizotolewa na Serikali upande wa Maendeleo ya Afya wanazisimamia vizuri.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike anafanya ziara ya ukaguzi wa Huduma za Afya na Vifaa Tiba Wilaya zote za Mkoa huo  ambapo tayari amezikagua Wilaya tatu za Kwimba,Sengerema na Misungwi na kutoa maagizo ya utekelezaji wa changamoto alizozibaini.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 05, 2021
  • Tangazo kuhusu uhamisho wa ndani na nje ya Mkoa wa Mwanza. January 05, 2021
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA MWANZA MWAKA 2021 February 05, 2021
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2018 Shule za Sekondari za Serikali Mkoa wa Mwanza December 13, 2017
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC Mwanza azindua msimu wa manunuzi zao la Pamba 2022/2023,atangaza bei elekezi Shilingi 1560

    May 20, 2022
  • RAS Mwanza afanya ukaguzi Sekta ya Afya Wilayani Ukerewe,ahimiza umakini kazini

    May 18, 2022
  • RC-MWANZA Azindua Chanjo ya Matone ya Polio Ukerewe

    May 18, 2022
  • Mkuu wa Mkoa Mwanza azikumbusha Familia kuzingatia wajibu wa Malezi kwa watoto

    May 15, 2022
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Regional Drive Mkabala na Ofisi za TRA

    S.L.P: S.L.P. 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.