RAS MWANZA ATAKA UHAMASISHAJI CHAKULA CHENYE LISHE KUONGEZEKA SHULENI
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Balandya Elikana amewataka wataalamu na wadau wa lishe mkoa kuongeza jitihada ili chakula kipatikane shuleni na kuweza kuboresha ufaulu na maendeleo bora.
Ametoa wito huo leo tarehe 13 Mei, 2025 wakati akifungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe ngazi ya Mkoa kwa kipindi cha Oktoba - Disemba, 2024 uliowakutanisha wataalamu na wadau mbalimbali.
Ameeleza kuwa mwezi Mei na Juni uhamsishaji utafanyika katika wilaya za ukerewe na Magu na ameziagiza shule kuwa na maeneo kwa ajili ya kilimo kwa lengo la kuzalisha mazao yao wenyewe.
"Tutajigawa ili twende kwenye baadhi ya maeneo kuhamasisha upatikanaji wa chakula mashuleni", amesema ndugu Balandya.
Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Jesca Lebba ameeleza kuwa suala la wanafunzi kupata chakula chenye lishe ni muhimu sana kwa kila mwanafunzi na akatoa wito kwa wazazi kushirikiana na serikali kufanikisha upatikanaji wa vyakula shuleni.
Aidha, ameshauri kwa halmashauri kupanga bajeti na kuitekeleza ili kuwezesha watoto wa shule kupata chakula wakati wa masomo na kushirikiana na wadau.
Kwa upande wa wadau hao wameshauri Kamati ya Lishe Mkoa kufanya juhudi za binafsi kutafilia na kuwekea mkazo na nguvu katika swala la kutungwa kwa sheria kwa wazazi na walezi wa wanafunzi Ili kuweza kuhamasisha katika upatikanaji wa chakula mashuleni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.