• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS Mwanza awapa kongole Agha Khan foundation kwa Mchango Sekta ya Lishe

Posted on: August 31st, 2023

RAS Mwanza awapa kongole Agha Khan foundation kwa Mchango Sekta ya Lishe


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Daniel Machunda amewashukuru Agha Khan foundation kwa michango wanayotoa kwenye jamii kwa kushirikiana na Serikali katika upande wa sekta ya lishe huku akibainisha kuwa serikali inawathamini kwa dhati.

Ametoa pongezi hizo mapema leo Agosti 31, 2023 wakati akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe ya Mkoa kilichoketi mahsusi kwa ajili ya kupitia na kusikiliza shughuli za Lishe ili kubainisha maeneo yanayohitaji usaidizi kwa ufadhili wa Shirika la Agha Khan foundation.

"Shirika la Agha Khan lina mchango mkubwa sana katika masuala ya Lishe na Sekta ya afya kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za matibabu kwa ujumla, watumishi wa afya tunapaswa kuunga mkono juhudi hizo kwa kushirikiana nao kwa karibu sana". Amesema Machunda.

Aidha, ametoa wito kwa wataalam kwenye Sekta ya lishe kuendelea kutoa elimu kwenye jamii kupitia makundi mbalimbali kuanzia ngazi ya Kaya, jamii na hata makundi ya kijamii na ili kuhakikisha suala la lishe linakua Agenda ya kudumu ili kujenga jamii iiliyoimarika kiafya.

Afisa Lishe Mkoa, Bi. Sofia Lazaro amefafanua kuwa Serikali inaendelea kuimarisha eneo la lishe nchini ndio maana Mhe. Rais anasaini Mkataba wa Lishe kwa Wakuu wa Mikoa ili kutekeleza afua za upatikanaji wa chakula chenye Lishe shuleni, upangaji na utoaji wa fedha za lishe kwa watoto chini ya miaka 5 na afua zingine.

Vilevile, amefafanua kuwa wanaume kutohusishwa kwa karibu kwenye masuala ya lishe, hali duni ya usalama kwa watoto, uelewa finyu wa jamii kwenye masuala ya lishe, lishe duni kwenye Kaya, unyonyeshaji usiofaa, mazingira magumu ya kijiografia ni matatizo yaliyopelekea utapiamlo kwenye jamii kwa muda mrefu na kwamba ni sehemu zinazofanyiwa kazi kwa karibu zaidi.

Meneja wa Afya na Lishe kutoka Agha Khan foundation David Siso ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na ameimwagia sifa Ofisi ya Mkua wa Mkoa wa Mwanza kwa kutekeleza afua za lishe kwa njia ya ushirikishaji wa pamoja ambayo amebainisha kuwa inasaidia kufikia malengo kwa wakati.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.