• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RAS- Mwanza, “PlanRep Mpya, Rafiki wa Mwananchi”

Posted on: July 24th, 2017

Serikali mkoani hapa imesema, Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ulioboreshwa utakuwa msaada kwa Mwananchi kwani utaweza kumshirikisha moja kwa moja wakati wakuibua vipaumbele vya maendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, C P. Clodwig Mtweve, wakati akifungua mafunzo  ya siku nane yaliyo andaliwa na TAMISEMI kupitia mradi wa Wamarekani wa kuimarisha mifumo yaani PS3 kwa watendaji wa Serikali kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala msaidizi upande wa uchumi na uzalishaji, Johanes Bukwali, amesema mfumo mpya wa PlanRep uliboreshwa unaenda kutumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vyetu vya kutolea huduma ambapo utawezesha kuandaa mipango na bajeti kutokana na vipaumbele na mahitaji ya wananchi.

Ameongeza kuwa,” kwa kutumia mfumo wa zamani wa PlanRep, ulikuwa huwezi kuainisha mipango na bajeti za kituo kimoja kimoja kwa kuwa mipango yote ilikua ikiishia kwenye ngazi ya Halmashauri, hali ambayo ni tofauti na sasa katika mfumo hu mpya wa PalnRep”.

Bukwali amesema kwamba, PlanRep iliyoboreshwa imefanyia kazi changamoto zilizokuwepo kwa kuhakikisha kwamba mpango na bajeti unaingizwa kwa kila mtoa huduma, na unaingiza namba za utambulisho kwa kila mtoa huduma mmoja mmoja kwa kila sekta. Vile vile, mfumo huu umeweka nafasi ya kila mtoa huduma kuainisha matokeo yaliyotarajiwa (Service Outputs), amesisitiza Bukwali.

Bukwali amemalizia kwakuwashukuru sana PS3 kwa mafunzo hayo, maana kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao tayari wamekuwa wanafanya kazi kwa karibu sana na Serikali ya Tanzania.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Elisa Rwamiago, amewataka washiriki hao kujifunza kwa umakini na kuulewa mpango huo ili katika mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018 waweze kuutumia katika kuandaa Bajeti zao.

Awali akizungumza Mwakilishi kutoka PS3 Desderi Wengaa, amesema wao kama PS3, ambao wanafanya kazi katika Mikoa 13 na Halmashauri 93 nchini, wanachotaka kuona ni matokeo chanya kwa kile wanacho kifanya.

“Mfumo mpya wa PlanRep ni wa kitaifa na uko kwenye toleo la mfumo wa kielektroniki ambao unatambulisha teknolojia ya mawasiliano na kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi mahali kokote na muda wowote” alisema Desderi.

 

Ameongeza kuwa, Mipango na bajeti za vituo vya kutolea huduma kwa wananchi itaonekana kupitia mfumo wa PlanRep kwa kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.  

Aidha amefafanua kuwa PlanRep itatumika katika sekta zote za umma na imehuishwa na mifumo mingine ya Serikali ili kuboresha usimamizi na kuwezesha Serikali katika ngazi zote kuweza kufanya kazi vizuri ili kutoa huduma bora kwa jamii.

Mafunzo  hayo kwa awamu ya kwanza yanafanyika katika kanda mbili, za Mwanza pamoja na  Mtwara, na kwamba yanajumuisha watumiaji wa mifumo hiyo ambao ni Waganga Wakuu, Makatibu wa Afya, Maafisa  TEHAMA na Wachumi kutoka ngazi ya Mkoa kwa upande mmoja, pamoja na  Waganga Wakuu, Maafisa Mipango, Wahasibu, Wachumi, na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri kwa upange mwingine,  ambao wahusika katika kuandaa mipango na bajeti za Halmashauri kutokana na taarifa zilizokusanywa kutoka vitengo mbalimbali ndani ya Halmashauri zao.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI MWANZA

    May 10, 2025
  • SERIKALI KUNUNUA MTAMBO RASMI WA KUSAFISHA ZIWA VICTORIA

    May 10, 2025
  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.