RC MAKALLA AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE TUKIO LA MOTO ISENI JIJINI MWANZA
*Aagiza Jeshi la Polisi kumsaka popote alipo Mhalifu wa tukio hilo*
*Awataka Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa kulinda Usalama kwenye Jamii*
Jioni ya leo Disemba 07, 2023 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amefika kwenye familia ya Marehemu Bi. Eva Yona Stephano Mtaa wa Ihushi kata ya Lwanima aliyeuawa pamoja na wanae wawili kwa Moto ndani ya nyumba yake usiku wa kuamkia leo jambo lililofanywa na mtu asiyejulikana na kutokomea.
Akiongea na familia hiyo Mkuu wa Mkoa ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo baya mara moja na mara tu akipatikana mhalifu huyo achukuliwe hatua kali za kisheria na ameahidi kwamba kama tukio hilo limefanywa na binadamu basi ni lazima akamatwe na kuadhibiwa.
"Kama ni binadamu mmoja au kikundi wamepanga njama kuchoma Moto huu, tupo kwenye msako mkali na lazima tutamkamata tu mhalifu, nanyi wenyeviti wa Serikali za Mtaa kuweni na tabia ya kutoa taarifa ya viashiria vya uhalifu au migogoro ya kifamilia kwa haraka ili kuzuia maafa kama haya yasitokee." Amesema kwa uchungu, Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.