RC Makalla ampokea Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla leo amempokea Ofisini kwake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ali Khamis ambaye yupo Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Katika mazungumzo mafupi Naibu Waziri huyo ameomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia kwa Maafisa ustawi wa Jamii kusimamia vyema vitendo vya ukatili kwa watoto ambavyo vimekuwa vikashamiri.
"Mhe.Mkuu wa Mkoa kuna tabia ya watoto chini ya miaka 18 kutumika kwa shughuli za miziki hii siyo sawa na adhabu yake ni faini ya Shs 500,000 au kifungo,"amefafanua Mhe.Mwanaidi.
CPA Makalla amemshukuru kiongozi huyo mwandamizi wa Wizara kwa kufanya ziara hiyo ambapo atatembelea pia kambi za wazee na watoto na makundi maalum na changamoto zake ataweza kuzibaini na kuzifanyia kazi.
Naibu Waziri pia ameikumbusha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwa tarehe Mosi Octoba ni siku ya wazee hivyo litumike jukwaa hilo kuzibaini changamoto zao ikiwemo suala la matibabu ya bure na vipaumbele vingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.