• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Makalla awataka wamiliki wa Bar na Hotel kuendesha shughuli zao pasipo kuathiri Jamiii inayozunguka

Posted on: May 26th, 2023

*RC MAKALLA AAGIZA KUFUNGULIWA KWA  BAR  NA HOTEL ZILIZOFUNGWA NA NEMC  MWANZA

- 

-AWAPIGA  stop NEMC ukamataji wa kutumia nguvu wamiliki wa  Bar na kuzusha tafrani kwa wateja


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla ameagiza kufunguliwa kwa Bar na Hotel zote zilizofungiwa na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) kwa kosa la kufungulia muziki mkubwa na kuweka utaratibu wa haraka wa kuelimisha makundi hayo.

Mhe. Makalla ametoa agizo hilo mapema leo ijumaa Mei 26, 2023 wakati wa kikao chake na wamiliki na wafanyabiashara wa bar na hotel mkaoni humo kilichifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

"Bar na hoteli hizi zikisimama, ajira zitasimama, biashara zitasimama na uchumi utasimama na tujiulize watawezaje kulipa faini wanazodaiwa wakati biashara wamefunga hawafanyi tena." Amesisitiza Makalla.

Makalla amepiga pia marufuku ukamataji wa nguvu huku akibainisha kuwa wafanyabiashara hao sio majambazi hivyo wanapaswa kuelimishwa wanapokosea kwa kuangalia uhalisia wa maisha kwani kuua biashara ni rahisi sana kuliko kuijenga.

Aidha, amewataka NEMC na wafanyabiashara waliopigwa faini kuketi pamoja na kuzungumza namna ya kumaliza matatizo hayo ili kuhakikisha biashara hazisimami kwa sasa na amewataka watulie na kuondoa hofu kutokana na tafrani za kamata kamata.

"Nataka NEMC watoke kwenye kuwa taasisi ya kamata kamata na kuwa kama chuo kwa kuwaona wadau wao kama watoto na wao kuwa walezi na wajikite kwenye kutoa elimu ili watambue nini wanapaswa kufanya na kitu gani hawapaswi kufanya." CPA Makalla.

Akisoma risala kwa niaba ya wafanyabiashara hao, Richard Lomweti amesema operesheni inayofanywa na NEMC kwenye bar na kumbi za starehe kuanzia Mwezi Mei 2023 imewaumiza kwa kuwapiga faini kubwa kwa kudai kuwa wanazalisha kelele tena bila kutoa elimu kwao hususani wakati wa kutoa leseni.

"Kifaa wanachotumia NEMC kinaonekana hakina uhalisia wa vipimo kwani hata muziki ukizimwa kinaonesha muziki umezidi kiwango na pia kinahusisha hata kelele zingine nje ya muziki husika kuwa ni kelele za muzuki." Amesema bwana Lomweti.

Aidha, amefafanua kuwa faini wanazotozwa na NEMC pamoja na adhabu za kuwekwa ndani au kizuizini zimekuwa kubwa tofauti na uhalisia wa kosa hivyo wametoa wito kwa taasisi hiyo kuondoa faini hizo zinazowaumiza kiuchumi.

Vilevile, wameomba NEMC kuketi nao kwa pamoja kuzungumza na kuona namna ya kuboresha huduma hizo pasipo kubughudhi na kwamba wafute faini zote na kufuta sheria kandamizi zisizoendana na mazingira halisi ya uchumi wa sasa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.