• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC Malima akabidhiwa Hati ya Makabidhiano na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel

Posted on: August 4th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima  Agosti 03, 2022 amekabidhiwa Hati za Makabidhiano na aliyekua Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Robert Gabriel kama ishara ya kukabidhiwa Rasmi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuanza Rasmi majukumu kwenye Mkoa huo.

Akizungumza na Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali amemshukuru aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Robert Gabriel kwa ushirikiano aliouonesha kwake kwa kipindi kirefu katika maeneo mbalimbali ambayo amekutana naye na kwa upendo wake kwa wananchi wa Mwanza aliokua akiwaongoza.

Mhe. Malima ametaja Ulinzi na Usalama Imara kuwa ni kipaumbele chake, uchumi na ustawi wa jamii katika maendeleo ya sekta za Elimu na Afya vikienda sambamba na uimarishaji wa Ukusanyaji wa Mapato ya ndani na kwamba vitakua vipimo vya maendeleo ndani ya Mkoa huo.

"Ndugu viongozi na watumishi tukitoka hapa leo tunaanza kufanya tathmini ya Maendeleo na Ustawi wa wananchi wa Mkoa wa Mwanza, Mwanza ni kubwa sana kiuchumi na hata kijamii hivyo inastahili mazuri zaidi ya ilivyo sasa kwahiyo naomba tukajipime katika hilo." Amesema Mhe. Malima.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Elikana Balandya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua na amebainisha kuwa yupo tayari kushirikiana kwa dhati na viongozi na watumishi wote katika kuuletea maendeleo Mkoa wa Mwanza.

Akitoa neno la shukrani, aliyekua Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ndugu Ngusa Samike ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumbadirisha kituo na amemhaidi kwenda kuchapa kazi kwa dhati.

Aidha, amemshukuru Mhe. Robert Gabriel kwa ushirikiano na miongozo mbalimbali na amewashukuru Viongozi wa Dini, Chama Cha Mapinduzi, Serikali na watumishi wote kwa kuuletea sifa na heshma Mkoa wa Mwanza kwa pamoja wakati wote waliohudumia wananchi kwa pamoja.

Naye, Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amemshukuru kwa dhati Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuwahudumia wananchi wa Mwanza na amewashukuru viongozi wa dini na amewasihi kuendelea kumuombea Mhe. Rais na Taifa ili liweze kupiga hatua kimaendeleo.


Vilevile, Mhe Gabriel ametoa rai kwa Viongozi na Watumishi wa Umma kumuomba Mungu wakati wote, kupenda Taifa lao na kumpenda Rais na kumuombea mema ili kupata mafanikio na kuweza kusaidia wananchi walio wengi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.