Aga khan Development Network kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada (Global Affairs Canada) kupitia mradi wa Improving Access to Reproductive Maternal and Newborn Health (IMPACT)Mwanza wametoa vifaa kinga vya kukabiliana na maambukizi ya Corona vyenye thamani ya Million 572,272,498.
Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, Meneja Mradi wa IMPACT Mwanza Edna Selestine amesema fedha hizo zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba ,vitendea kazi pamoja na kuwezesha mafunzo ya watoa huduma za afya juu ya ugojwa huo pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii jinsi ya kuendelea kuelimisha jamii kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi .
Anasema vifaa hivyo vimenunuliwa kwa ushirikianao wa ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza hapahapa Nchini huku msaada huo ukiwalenga watoa huduma za afya na vituo vya kutolea huduma za afya mkoani humo.
Selestine amevitaja vifaa hivyo kuwa ni PPE,150 sets,Barakoa N95 750pcs, Chlorine tablets 100TB -300,surgical masks 35000pcs,Gloves examination,15000pairs na Gloves surgical 3500 pairs,vitakasa mikono 75lts,vitanda vya wagonjwa 30 na magodoro yake pamoja na mabegi 717 ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Aidha Agha Khan inapongeza juhudi zilizofanya na Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa namna alivyokabiliana na vieusi vya corona hadi kufikia hii leo ambapo maambukizi yamepungua kwa kiasi kikubwa.
"Tunatambua kupitia Wizara ya afya kuwa maambukizi ya ugonjwa wa Corona yamepungua nchini pia tumehimizwa kuendeleza jitihada zote za kuendelea kujilinda, mradi wa IMPACT utaendelea kushirikiana na mkoa kila inapowezekana ili kuhakikisha gonjwa hili linatokomezwa kabisa na afya za wananchi zinaendelea kuwa salama" alisema Selestine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza baada ya kupokea msaada huo amesema wamekuwa wabia na taasisi hiyo na wameweza kujenga majengo 28 katika vituo vya afya vya sehemu mbalimbali kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto pia vitanda thelathini walivyotoa kwa ajili ya mapambano ya Corona amevigawa 10 Ilemela,Nyamagana 10 na Buchosa 10.
Vilevile aliendelea kuwasihi wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya wizara ya afya ,maombi,kutumia miti shamba iliyodhibitishwa sambamba na kupinga nyungu .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.