RC MTANDA AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUONGOZA KUPATA FAIDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amefanya mazungumzo na Meneja mpya wa Kanda ya ziwa kutoka benki ya NMB Bi. Faraja Ngingo
na kuipongeza Taasisi hiyo kwa kuwa kinara wa kupata faida nchini ya shs bilioni 644 baada ya kukatwa kodi.
Akizungumza na mgeni huo ofisini kwake leo tarehe 30 januari, 2025 Mtanda amebainisha kuwa kufanya vizuri kwa taasisi hiyo kunazidi kuwapa imani wateja wake na kupiga hatua kiuchumi.
"Hongereni sana natambua Serikali nayo ina hisa ya 31% mkakati yenu ya kuinua uchumi wa Taifa ni mizuri ikiwemo utoaji wa mitaji mikubwa ya mikopo kwa wafanyabiashara huku mkiwa wabunifu kwa wafanyabiashara wadogo na Ile mikopo isiyolipika ikishuka kwa asilimia 2.9,ni dhahiri NMB ni benki ya mfano wa kuigwa," Mtanda.
Aidha ametoa ushauri kwa benki hiyo kuzidi kutanua wigo wa ubunifu wa kulisaidia kundi kubwa la vijana kwa kuwaongezea mitaji ya mikopo hasa kutokana na fursa zinazoanza kuja mkoani Mwanza mara baada ya miradi ya kimkakati kukamilika
"Kwa mwaka huu tumetenga shs bilioni 6.4 ambazo zitakwenda kusaidia shughuli za afya na elimu huku tukiendelea na mpango wetu wa kuwadhamini wanafunzi 65 kila mwaka waliopata ufaulu wa daraja la juu na wanaotoka kwenye kaya masikini kwa masomo ya elimu ya juu," Bi.Faraja.
Amesema mara baada ya mkutano wa kimataifa wa wadau wa nishati ya umeme kumalizika Jijini Dar-e-s-Samaam,benki ya NMB kwa kutambua mnyoroeo wa thamani kwenye eneo hilo, imetenga shs bilioni 100 na itatoa mkopo wa shs bilioni 1 kwa mtu watakao jishughulisha na nishati ikiwemo na uuzaji wa gesi.
Benki ya NMB mwaka 2024 imepata faida ya shs bilioni 931 na baada ya makato ya kodi imepata shs bilioni 644.
Wakati huo huo uongozi wa benki ya maendeleo ya kilimo TADB Kanda ya ziwa umesema mwaka 2024 umetoa mkopo wenye thamani ya shs bilioni 38 kwa makundi ya kilimo cha mazao,mifugo na uvuvi
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyefika Ofisini kwake kutoa salamu za mwaka mpya,Meneja wa benki hiyo Alphonce Mokoki amesema upande wa uvuvi vi wametoa boti 55 zenye thamani ya shs bilioni 2.5 na vizimba 222 vilivyogharimu shs bilioni 6.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.