• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AKABIDHI GARI JIPYA KWA WANACHAMA CWT SENGEREMA

Posted on: July 15th, 2024

RC MTANDA AKABIDHI GARI JIPYA KWA WANACHAMA CWT SENGEREMA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo  15 Julai 15, 2024 amekabidhi gari jipya aina ya TATA lililogharimu Shilingi Milioni 145 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wanachama wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Jiji la Mwanza  Mhe. Mtanda amewataka CWT kuhakikisha wanaajiri dereva muadilifu na mwenye weledi ambaye atalitunza gari hilo kwa muda mrefu.

"Gari hili ni la gharama kubwa sana  hivyo lazima mlitunze, msiajiri dereva mlevi mwisho wake akaligongesha na akawasababishia hasara". Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.

Amesema, gari hilo ni lazima litumike kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kuimarisha mahusiano baina ya walimu kutoka wilaya moja na nyingine kupitia kutembeleana kwa shughuli za kitaaluma pamoja na michezo mbalimbali.

Awali, Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Mwanza Mwalimu Lameck Mahewa alibanisha kuwa fedha zilizonunua basi hilo ( Milioni 145) zimetokana na michango ya wanachama wenyewe.

"Tunashukuru sana kupata gari hii, nina imani pia litatumika kuwapeleka uwanjani walimu mashabiki wa timu ya pamba pale Pamba Jiji itakapokuwa ina chuana hapa Mwanza". Mwalimu Mahewa.

Gari hilo linatazamiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa chama cha walimu Wilaya ya Sengerema katika kufuatilia maslahi na madai mbalimbali ya walimu ndani ya wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza na hata ngazi ya Taifa.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RAS MWANZA ATAKA UHAMASISHAJI CHAKULA CHENYE LISHE KUONGEZEKA SHULENI

    May 13, 2025
  • RC MTANDA AIPONGEZA BONDE LA ZIWA VICTORIA KWA KUELIMISHA UMMA

    May 13, 2025
  • RC MTANDA ASISITIZA UIMARISHWAJI WA UMOJA NA MSHIKAMANO

    May 12, 2025
  • SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI MWANZA

    May 10, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.