Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Februari 20, 2026, amempokea ofisini kwake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, Mhe. Deus Sangu, aliyefika kutoa salamu kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Mhe. Sangu yupo mkoani Mwanza kushiriki hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya udereva wa pikipiki na bajaji. Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mhe. William Kafiti kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mwanza pamoja na Benki ya CRDB.

Ziara hiyo inalenga kuhamasisha ajira na kuwajengea vijana ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuongeza kipato chao kupitia sekta ya usafirishaji.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.