RC MTANDA ASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameahidi kutatua kero za wananchi wa Mwanza kwa kutumia sheria, kanuni na taratibu ili kuepusha mgongano wa kisheria hususani kwa kero zilizopo Mahakamani.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza leo Jumanne Mei 14, 2024 Mhe. Mtanda amesema serikali inaweza kusikiliza na kusuluhisha kero na migogoro kwa kutumia njia badala ya kwenda mahakamani naye akajipambanua kusimamia hayo.
Aidha, amejipambanua kuhakikisha anamaliza migogoro kwa kutumia njia ya kuwasikiliza na akaahidi watakaomuelewa vema watamaliza kero zao kwa muda mfupi kwa usaidizi wa wataalamu wake tofauti hata na ilivyo kwa kesi zinazochukua muda mwingi mahakamani.
Amesema sheria, kanuni na taratibu zitafuatwa kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwenye nayo na kwamba akawataka kujiepusha na kuibua kesi ambazo zilishatolewa maamuzi na wakuu wa Mkoa huo waliopita kwani hayuko tayari kupindisha maamuzi ya awali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.