• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AWAPONGEZA JWTZ MWANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE

Posted on: August 28th, 2024

RC MTANDA AWAPONGEZA JWTZ MWANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda  amelipongeza Jeshi la wananchi wa Tanzania Mkoani humo kwa kuweka kambi ya matibabu bure ikiwa ni katika kuadhimisha miaka 60 ya jeshi hilo.

Pongezi hizo zimetolewa leo Agosti 28, 2024 mara baada ya kukagua mabanda ya kambi ya matibabu yaliyopo viwanja vya Furahisha Manispaa ya ilemela.

"Ninakupongeza Luteni kanali pamoja na wenzako kwa kuadhimisha miaka 60 ya jeshi kwa kutoa huduma za afya kwa wananchi wetu  pamoja na kuendelea kuimarisha ulinzi ambalo ndio jukumu lenu". Amesema Mhe. Mtanda.

Aidha Mhe. Mtanda amewataka Wananchi kuendelee kushirikiana na serikali kwani serikali inaendelea kuboresha huduma za afya nchini na nia kubwa ni kutibu wananchi hivyo amewataka wananchi kufika kwenye hospitali ya jeshi pale Ilemela kwani kuna vifaa vya kisasa.

Sambamba na hayo pia Mhe. Mtanda amewatoa hofu wananchi wote wanaoendelea kuzuru katika viwanja hivyo kuwa watapatiwa huduma na hakuna yoyote kati yao atakayeachwa kwani Jeshi limemhakikishia hilo na kutoa rai pia kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi.

Naye Luteni kanali Ahmedi Ali Shabhay amesema kama Hospitali ya Kanda ya Jeshi wamejipanga vyema kuhakikisha wanawahudumia wananchi wote watakaojitokeza, aidha amesema pia wamekua na ushirikiano kwa karibu na Wataalamu kutoka Damu salama na hivyo kupelekea kuwepo kwa huduma ya uchangiaji damu katika viwanja hivyo.

Aidha Luteni Kanali Shabhay ametumia wasaa huo pia kutoa wito kwa wananchi kufika katika hospitali ya jeshi ya kanda ya ziwa Magharibi iliyopo Mtaa wa Uwanja wa Ndege Wilayani Ilemela kwani wanatoa huduma mbalimbali za afya na amewakaribisha kufanyiwa uchunguzi na matibabu katika hospitali hiyo ambayo inahudumia wananchi wote.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.