Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda, amezindua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Bumyengeja iliyopo Kata ya Sumve, Wilaya ya Kwimba. Shule hiyo ni mpya, iliyoanza mwaka 2024, ikiwa na wanafunzi 227, kati yao wasichana 150 na wavulana 77, pamoja na walimu 16 ambapo 13 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Shule ina jumla ya madarasa nane, jengo la utawala, maabara tatu, maktaba na chumba cha TEHAMA. Miundombinu hiyo imelenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wa eneo hilo na vijiji jirani.

Katika mapokezi ya fedha mnamo Juni 30, 2023, Shule ya Sekondari Sumve ilipokea Sh. 584,280,028.00 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya. Ujenzi ulianza Agosti 14, 2023 na shule ilianza kutumika rasmi Januari 2024.

Aidha, Juni 24, 2024 shule ilipokea Sh. 100,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu (2 in 1). Mradi huo ulianza Septemba 30, 2024 na kukamilika Januari 2025. Miradi hiyo imefadhiliwa kupitia mpango wa Secondary Education Quality Improvement Program (SEQUIP).

Mradi wa Shule ya Sekondari Bumyengeja umeleta manufaa makubwa kwa jamii kwa kupunguza umbali wa wanafunzi kwenda shule, kupunguza utoro na mimba za utotoni, kupunguza msongamano katika shule mama ya Sumve, na kuboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya elimu katika Kata ya Sumve.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.