Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi ameagiza ujenzi wa zahanati kwa vijiji 74 vilivyopo wilayani Kwimba,mkoani Mwanza visivyokuwa na huduma hiyo zijengwe ili wananchi wapate huduma kwa kila Kijiji.
Hayo ameyabainisha leo mara baada ya kupitia hoja za mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2019 hadi 2020,ambapo amewaagiza maofisa tarafa kwenye maeneo yao waitishe kikao na watendaji wa kata na vijiji ili kila Kijiji kipate ramani na wajilidhishe na eneo ili zoezi la ujenzi wa msingi wa zahanati kwa kila Kijiji uanze.
"Naomba muyabebe haya maagizo kwa sababu nyie ndio mnaomsaidia Mkuu wa Wilaya kwenye kata zenu ,tutafute mchanga na mawe na mimi nitakuja kuzunguka kata zote tunataka mwaka 2025 wakati Katibu wetu wa chama anasimama kwenye jukwaa anawanadi madiwani awe anasema tuliahidi tunatekeleza," amesema na kuongeza
"74 ni idadi kubwa mno huko nilipotoka kazi imeanza maboma yanakwenda kwa hatua mbalimbali,nimetoka Buchosa wanaupungufu wa zahanati 24, Sengerema 30 hapa 70 vijiji vyote hivyo wananchi wanahitaji huduma nitakuja kwenye kata na tarafa zenu zote Mwenge wa uhuru ukiondoka mimi naingia saiti tutakutana ili tujue kazi inaendeleaje tulishafanya majaribio hayo ikakubali na hapa itakubali,"alieleza Mhandisi Luhumbi.
Pia amesema,andiko la mradi liandikwe kwa kiswahili na wasimfiche mtu kwa lugha ya kiingereza ili ashindwe kuelewa,lengo ni kuboresha wapo kwenye mapambano ya kuleta maendeleo.
Aidha amewataka wataalamu kuonesha thamani ya fedha na wataenda kukagua majengo kama wamepigwa ama hawajapigwa kwa sababu wanajua hiyo inatokana uzoefu,endapo kunamtu mzembe asiyefanya kazi wamuweke pembeni kwani maendeleo lazima yaende mbele .
Amesema kikubwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa,wanahitaji kufanya mapinduzi katika usimamizi wa miradi,amepitia hizo hoja lazima awe muwazi kwa hoja mpya 2019/ 2020 wamefanya vizuri.
"Millioni 80 nimejenga shule ambapo kwenye BOQ ni vyumba vinne mimi nilijenga shule mpya ya msingi yenye vyumba vya madarasa saba na ofisi mbili lazima tutumie vizuri fedha ya umma inayokuja,lazima tuwe na mawimbi ya maendeleo pia madiwani watafute ardhi ambayo wanaweza kuwekeza miradi ambayo 1wanaweza kupata mapato mazuri kama kuanzisha majengo ya biashara ili kuchochea maendeleo,"alieleza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.