Serikali imepongezwa na Shirika la Under The Same Sun kwa namna ilivyoshiriki kupunguza mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi tangu 2008 hadi 2018 ambapo matukio yamepungua kutoka 40 kwa mwaka na kufikia nane.
Shirika hilo limesema licha ya mauaji kupungua kwa asilimia 90 bado kundi hilo linakumbwa na vitendo vya unyanyapaa na kutopewa nafasi ya ajira ambapo jamii imekuwa ikiwaita majina mbalimbali ya kebehi yakiwamo ya wanyama.
Akizugumza na waandishi wa habari jana katika kambi ya wiki moja iliyowekwa katika Chuo cha Walimu Butimba jijini Mwanza iliyopewa jina la ‘Summer Camp 2019’, Muasisi wa Shirika hilo kutoka Canada, Peter Ash alisema ni mafanikio makubwa kwa shirika na Serikali kufikia hatua ya albino kuisha bila hofu.
“ Mauaji au matukuo yamepungua sana, mfano tangu mwaka 2008 matukio yalikuwa 40 kwa mwaka lakini yameendelea kupungua hadi kufikia nane mwaka jana, mpaka tunavyozungumza sasa kwa mwaka huu wa 2019, matukio yameripotiwa mawili tu.
“Jambo ambalo badi linaonekana linaendelea ni unyanyapaa na kutopatiwa fursa ya ajira, wapo watu wanawaita majina ya wanyama kama mbuzi, nguruwe na majina mengine ya kikabila suala hili tunaendelea kutoa elimu kwa jamii, pia vitendo vya baba kutelekeza familia kutokana na mama kujifungua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi vimepungua na sasa wanawalea.
“Hapo awali kulikuwa na mtazamo kwamba watu wenye ualbino hawafariki bali wanapotea tu, vile vile mitazamo ya jamii ilikuwa kwamba ukimgusa ni kosa hivyo hivyo ilionekakana mama akijifungua mtoto wa namna hiyo ni mkosi lakini leo wanashirikiana kwa kula na kulala pamoja, jambo ambalo tunalisisitiza kupewa ajira, inaweza kutokea kuna nafasi lakini ni ngumu kupewa licha ya kuwa na vigezo,”alisema.
Ash alisema alisema shirika hili liliamua kuja Tanzania kutokana na vitendo vilivyokuwa vikifanyika vya ukataji viugo vya albino kutokana na imani za kishirikiana ambapo kutokana na jitihada walizozifanya za utoaji elimu kwa jamii, wanajisikia faraja kuona uahueni imepatikana.
Aliongeza kuwa mpaka sasa kuna watu wenye ualbino 400 wanaolelewa na shirika hilo ambapo wale wanaosoma wanalipiwa ada, vifaa vya shule na kuwakatia kadi za afya kutoka Mfuko wa Taifa wa Afya (NIHF) huku akiwataka jamii kuelewa kuwa ualbino ni hali ya kawaida ya kurithi inayotoka kwa baba na mama.
Ash alisema kwa kipindi cha miaka 10 sasa amegundua kwmaba watu wenye ulemavu wa ngozi wana akili kubwa na ujuzi hivyo aliiomba Serikali na mashirika binafsi inapotokea fursa ya ajira kundi hilo litazamwe ili waweze kuwa sehemu ya viongozi.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun-Tanzania, Berthasia Ladislaus kambi hiyo yenye watoto 180 kutoka mikoa yote Tanzania bara watakuwepo hapo kwa lengo la kujifunza mambilimbali na kuonyesha vipaji.
“Watoto hawa wametoka mikoa yote na tumechukua 180 ingawa shirika linalea 400, hapa watafundishwa mambi mengi na kuonyesha vipaji, tumekuja hapa na wachungaji, watalaamu wa mambo mbalimbali wakiwamo wabebezi wa uandishi wa habari ili nao watoe elimu maana wapo watoto wanaopenda kuwa waandishi.
“Jambo ambalo tunasisitiza kwa jamii, mashirika ya binafsi na Serikali ni kwamba tunao vijana waliofikia vyuo vikuu na wanafanya vizuri sana, hivyo wapewa fura inapojitokeza ili na wao wawe viongozi katika ngazi za juu,”alisema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.