• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOKIUKA SERA YA CHAKULA SHULENI

Posted on: July 31st, 2024

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOKIUKA SERA YA CHAKULA SHULENI


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata na Viongozi wote wanaratibu na kusimamia sera ya chakula shuleni kuhakikisha wanaiendeleza sera ya kutoa chakula kwa wanafunzi pindi wawapo shuleni na wale ambao wanakiuka kampeni hiyo basi taarifa zitolewe ili waweze kuchukuliwa hatua.

Balandya ametoa tamko hilo Julai 30, 2024 alipokuwa akiongoza kikao cha kamati ya lishe ngazi ya Mkoa kilicholenga kuboresha afya kwa watumishi na wananchi, ambapo amewataka Viongozi hao wa afya ngazi ya Mkoa kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na Serikali ikiwemo kuisimamia kwa ufasaha sera ya chakula shuleni.

Aidha, Katibu Tawala huyo amewataka watumishi wa afya ngazi ya Mkoa kuhakikisha wanasimamia sekta ya mazoezi pia kwa kuwa ndio msingi wa afya imara na katika kusisitiza hilo ametaka kuwepo na vipindi maalumu vya mazoezi kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

"Mnaweza mkatenga hata siku tatu kwa wiki, kila siku mtakayoichagua jioni mara baada ya muda wa kazi mkawa na kipindi cha mazoezi kwa watumishi wa hapa ofisi ya Mkuu wa Mkoa". Amesema Balandya wakati akisisitiza kuhusu kufanya mazoezi.

Kadhalika Bw. Balandya ametumia kikao hicho pia kuwataka Viongozi hao wa afya ngazi ya Mkoa kuhakikisha wanatoa elimu ya matumizi sahihi ya chupa za maji za plastiki ambapo kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa kutumika tena huku zikiwa tayari zimeshatumika na kwa namna zilivyotengenezwa hazikupaswa kutumiwa tena na hivyo zinaweza kuleta madhara kwa afya.

"Niwatake pia mkatoe elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya chupa ambazo zimekwishakutumika ni hatari kwa afya, hivyo mkawaambie wananchi huko anaweza akaitoboa chupa hiyo mara baada ya kuitumia ili kuifanya chupa hiyo isitumike tena". Amesema Balandya.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.