Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amefunga soko la Mlango Mmoja kutokana na janga la moto lililotokea tarehe 28/09/2018 saa 10:30 alfajiri siku ya Ijumaa.
Akitangaza Agizo hilo la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ,Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Dkt Phillis Nyimbi amesema wakati huu wanalazimika kufunga soko kwa siku mbili kwa ajili ya wafanyabiashara kuendelea kufanya tathimini ya mali zilizoharibika chini ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Nyamgana amesema kwa wakati huu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya,Halmashauri ya Jiji la Mwanza, viongozi wa soko,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa siasa watakaa pamoja na kuja na mikakati ya muda mfupi,muda wakati na muda mrefu kwa ajili ya soko la Mlango mmoja.
Hata hivyo Dkt. Phillis Nyimbi ametoa shukrani kwa wadau wote wakiwemo Polisi, Zima moto,Nile Perch, Mwauwasa pamoja na wananchi walivyojitokeza na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa uliopelekea moto kudhibitiwa kutokuendelea kuleta madhara makubwa.
Moto ulianza kuwaka saa 10:30 Alfajiri ya leo kwenye mabanda ya mama lishe, na mafundi Cherehani na mabanda ya nguo na viatu.
Kwa taarifa ya awali ya kamati ya Tathimini imebaini kuwa maduka 23 kati ya 156 yameteketea na Meza 55 kati ya 351 zimetekea zenye mali yenye thamani ya Tsh 583,134,000.
Maduka Mengi yalikuwa yakitumika kama stoo ya wafanyabiashara wa Mlango mmoja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.