UHUSIANO WA TANZANIA NA UJERUMA NI UMEZIDI KUWA NA TIJA: RC MAKALLA
*Aishukuru Ujerumani kwa kuutambua Mkoa wa Mwanza Kimkakati na kuiumarisha kimaendeleo*
*Asema Miradi ya Maji, Afya, Mazingira inaendelea kupiga hatua*
Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala leo Machi 22, 2024 amempokea balozi wa Ujerumani hapa nchini Mhe.Thomas Terstegen na kusema uhusiano baina ya nchi hizo ulioanza tangu mwaka 1960 umekuwa na tija kutokana na kuwepo miradi mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Masala amebainisha kuwa miradi iliyoletwa na Ujerumani hususani sekta ya Afya, Umeme, Maji, MaliAsili na Elimu na mingineyo imekuwa chachu ya maendeleo hapa nchini.
"Mhe. Balozi nikushukuru kwa kuutambua Mkoa wa Mwanza upo kimkakati na kuleta miradi ya afya,maji na mazingira hii ni hatua nzuri ambayo itazidi kuumarisha kiuchumi mkoa huu," Mkuu wa Wilaya.
Balozi wa Ujerumani Mhe.Thomas Terstegen amesema uhusiano wa Tanzania na Ujerumani utazidi kuwa endelevu huku ukiwanufaisha wananchi wa pande zote mbili.
"Kutokana na jiographia ya Mwanza tutaleta Mradi wa kuimarisha mifumo ya maji taka na safi kwa wanaoishi sehemu za milimani, pia tutajenga kingo za mto mirongo na kuleta vifaa vya kupambana na uchafuzi wa mazingira." Balozi.
Balozi huyo katika ziara yake ya siku mojs Mwanza atatembelea pia Chuo cha wanyamapori cha Pasinsi, miongoni mwa miradi wanayoifadhili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.