• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Waajiri wababaishaji waonywa Mwanza

Posted on: May 1st, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.Adam Malima amesema waajiri wasiozingatia sheria za kazi watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za sheria.

Pia  amewataka  waajiriwa (watumishi )kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na uwadilifu.

Mhe.Malima ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2023 wakati  akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa  Wilayani Sengerema mkoani humo .

" Maagizo yangu kwa  waajiri zingatieni sheria za kazi ikiwemo kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati,"amesema Mhe.Malima.

Mhe.Malima ameongeza kuwa katika kujali maslahi ya watumishi Serikali ya Awamu ya Sita,mkoani Mwanza imewalipa sh.bilioni 1.74 watumishi 571 walioghushi vyeti na sh.milioni 660 walilipwa watumishi 503 za malimbikizo yasiyo ya mishahara.

"Kazi inayofanywa na Rais  Mhe.Dk.Samia Suluhu Hassan, ni kubwa,yapo maeneo itaendelea kujipanga kuboresha maslahi ya wafanyakazi na  kufanyia kazi nyumba za watumishi na stahiki zingine hatua kwa hatua," amesema Mhe.Malima.

Awali Mratibu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) mkoa wa Mwanza,  Zebedayo Athuman, alisema baadhi ya waajiri wanakiuka sheria,hawawasilishi michango ya watumishi kwenye

mifuko ya jamii,hawatoi mikataba ya ajira na hawalipi mishahara kwa wakati.

."TUCTA tunaiomba Serikali ifanyie kazi changamoto hizo ili kuwapa nafuu wafanyakazi na kukomesha tabia  za waajiri wasiozingatia sheria za nchi, " alisema Athuman.

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mwaka huu 2023  yameongozwa na kauli mbiu isemayo  'Mishahara Bora na Ajira za Stara ni Nguzo ya Maendeleo ya Wafanyakazi." Wakati ni sasa.




Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.