Wananchi hasa wavuvi watarajia kunufaika na huduma za d.light baada ya kuzindua ofisi ya Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Diwani wa Kata ya Nyamagana Bhiko Kotecha alisema ni wakati wa d.light kwenda kwenye mialo na kutoa elimu kwa wavuvi ili waachane na uvuvi wa kutumia taa za mafuta bali watumie d.light ili kuboresha mazingira na kuondokana na gharama kubwa wanazozitumia kwa sasa.
"Uwepo wa tawi hilo litawasaidia kufika kwa ukaribu nimeona bidhaa zenu ni nzuri na mpangilio wa uuzaji wenu ni mkakati mzuri kwa jamii ya hali zote hakika mnaleta mwanga na kuboresha maisha ya watanzania na hii ndio chachu ya maendeleo" alisema Kotecha
Saitoti Naikara ni Meneja biashara d.light Kanda ya Ziwa alisema mikakati ya kampuni hiyo ni kuhakikisha ifikapo 2030 wawe wamewafikia wateja zaidi ya Billion 1 ambao watakuwa wanatumia bidhaa zao hiyo inatokana na upatikanaji wake kuwa rahisi na zenye gharama nafuu zaidi na inampa mteja uhuru wa kuchagua kulipa kidogokidogo ana kununua kwa pesa taslimu.
Alisema malengo yao ni kuifikia jamii yote hasa maeneo ya vijijini ambayo yanakabiliwa na changamoto ya nishati mbadala ya uhakika pia wametoa ajira kwa vijana ambao ni mawakala sehemu mbalimbali lakini pia watawafikia wavuvi kwa sababu wana vifaa vinavyokaa na mwanga muda mrefu huku vikiang'aza zaidi ikiwa ni kuonyesha nia thabiti ya kuisadia serikali katika kupambana na uharibifu wa mazingira kuacha kutumia nishati ya mafuta kipindi cha uvuvi
Kwa upande wake Charles Budeba mmoja wa wateja wa d.light alisema anajivunia kuwa mteja wa kampuni hiyo kwani wanahuduma nzuri familia yake inanufaika watoto wamepata mwanga wa kusoma pia mfugo yake kutoshambuliwa na wanyama kama ilivyokuwa mwanzo kwa sababu ya giza .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.