Waziri Silaa ampongeza RC Makalla kwa kusimamia na kutatua migogoro ya ardhi Mwanza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa yupo kwenye ziara fupi Mkoani Mwanza na kumpongeza Mkuu wa Mkoa huo Mhe.CPA.Amos Makalla kwa kusimamia na kutatua vyema migogoro ya ardhi ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi.
Akizungumza leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi kutoka sekta ya ardhi, Mhe Silaa ameweka bayana kuwa huo ni mfano wa kuigwa kwa watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia eneo hilo kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria za ardhi.
"Migogoro mingi inaonesha dhahiri chanzo ni sisi baadhi yetu tunaopindisha taratibu zilizopo kwa tamaa binafsi na kuwaacha wananchi wakitaabika na kudhulumika, hilo kama Waziri mwenye dhamana sitalifumbia macho,"amesisitiza Waziri Silaa wakati akizungumza na watumishi kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara yake na wengine kutoka Halmashauri.
Amesema Mhe.Makalla amelazimika kutoka ofisini na kwenda kujionea kero zinazowarudisha nyuma kimaendeleo wananchi wake na kuzitolea maamuzi, nyingi zikiwa ni migogoro ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya watumishi waliokosa nidhamu ya kazi na badala yake kukimbilia kujinufaisha
"Haiwezekani sheria ziwekwe halafu wengine wanazitii na baadhi kuzipuuzia tena kwa kukusudia huo siyo utaratibu unaokubalika na nitahakikisha uzingatiaji wa sheria za nchi unaheshimika,"Silaa
Waziri Silaa ametoa maagizo kwa kamishna msaidizi wa ardhi Mkoa wa Mwanza Bi.Happines Mtutwa kuhakikisha mkazo wa elimu,ufuatiliaji,na utatuzi wa kero kwa wananchi unafanyika mara kwa mara
Awali kabla ya kikao hicho Waziri Silaa alipata wasaa wa kupata taarifa fupi za mkoa wa Mwanza hasa masuala ya ardhi kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi anaye kaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.