• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Waziri wa Madini Uganda atembelea Tanzania

Posted on: April 1st, 2019


Waziri wa Madini Nchini Uganda, Mhe. Peter Lokeris pamoja na ujumbe wake wameanza ziara nchini Tanzania leo tarehe 01 Aprili, 2019 yenye lengo la kujifunza namna sekta ya madini nchini Tanzania inavyoendeshwa. Waziri Lokeris ameongozana na maafisa waandamizi kutoka Serikali ya Uganda pamoja na wawakilishi wa wachimbaji wadogo. Waziri wa Madini Nchini Uganda pamoja na ujumbe wake walipokelewa na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo kupitia mahojiano maalum aliyoyafanya na vyombo vya habari, mara baada ya kupokelewa na Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Stanslaus Nyongo, Waziri Lokeris alisema kuwa lengo la ziara yake ni kujifunza sheria na kanuni za madini nchini Tanzania zinavyosimamiwa vyema pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini nchini Tanzania kwa vitendo kupitia wawekezaji waliowekeza nchini pamoja na wachimbaji wa wadogo wa madini.

“Tulifanya utafiti na kubaini Tanzania ni  nchi yenye utajiri mkubwa wa madini na uzoefu mkubwa kwenye uchimbaji wa madini na tumeona wachimbaji wadogo wakisaidiwa sana na Serikali ya Tanzania,” Alisema Mhe. Lokeris.



Aliongeza kuwa,  kati ya maeneo wanayotarajia kujifunza ni pamoja na ushirikishwaji wa wazawa kwenye  shughuli za uchimbaji wa madini (local content) utoaji wa huduma kwa jamii inayozunguka shughuli za uchimbaji wa madini (corporate social responsibility), usimamizi wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake.

Aliongeza kuwa ushirikiano wa Tanzania na Uganda umekuwa ni wa muda mrefu na kusisitiza kuwa Serikali ya Uganda ipo tayari kujifunza na kubadilishana uzoefu kwenye usimamizi wa sekta ya madini.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali ya Tanzania inapenda kuona wananchi wake hususan waishio vijijini wananufaika na sekta ya madini kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii kama vile elimu huduma za afya, na ili kuhakikisha wananchi wake wananufaika, Serikali imeamua kutuma wataalam wake Tanzania kujifunza kutokana na hatua kubwa iliyopigwa na nchi ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini.

Akielezea changamoto kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa nchi ya Uganda, Waziri Lokeris alieleza kuwa ni pamoja na kutokuwa na teknolojia ya kutosha kwenye uongezaji thamani wa madini pamoja na utoroshwaji wa madini unaofanywa na wachimbaji wadogo.

Wakati huohuo Naibu Waziri wa Madini Nchini Tanzania, Mhe. Stanslaus Nyongo alisema kuwa nchi ya Tanzania ipo tayari kutoa uzoefu wake kwenye usimamizi wa sekta ya madini kwa nchi ya Uganda kupitia wataalam wake.

Alisema katika ziara ya ujumbe huo, mbali na nchi ya Tanzania kutoa uzoefu wake kwenye usimamizi wa sekta ya madini nchini, wanatarajia kuupeleka ujumbe huo kwenye soko la madini mkoani Geita lililozinduliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya mitambo ya kuchenjulia dhahabu.

Akielezea mikakati ya Serikali ya Tanzania kwenye usimamizi wa sekta ya madini, Naibu Waziri Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na uboreshaji wa sheria ya madini pamoja na kanuni zake ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa wachimbaji wadogo wa madini.

Alieleza  mikakati mingine kuwa  ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini katika kila mkoa ili kudhibiti  utoroshwaji wa madini nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amewakaribisha na kuwahakikishia kuwa Tanzania watakuwa salama na watajifunza mengi kwani ni nchi iliyojipanga kimkakati katika madini.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.