MKUU WA MKOA MWANZA AWASHUKURU KANISA LA AICT UWEKEZAJI SEKTA YA AFYA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amelipongeza Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwa usimamizi na uendeshaji wa meli ya matibabu kwa kutoa huduma za afya
katika visiwa vya ziwa victoria kwa zaidi ya miaka 10.
Mhe. Mtanda ametoa pongezi hizo leo Februari 08, 2025 wakati wa Maadhimisho ya miaka kumi ya mpango wa meli ya matibabu ya MV Jubilee Hope Medical Ship na uzinduzi wa meli ya matibabu ya MV. Lady Jean yaliyofanyika katika viwanja vya Rock Beach Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa amewashukuru pia Washirika katika uendeshaji wa meli ya matibabu Vinetrust, (Geita Gold Mining Ltd – GGML), hivyo kufanikisha safari ya miaka 10 katika kutoa huduma za afya
katika visiwa vya ziwa victoria.
Sambamba na hilo ametoa shukrani za dhati kwa wadau wengine ambao ni Vine Trust UK kwa kushikiriana na Babcok kwa kufanikisha upatikanaji wa meli nyingine ya matibabu ambayo itasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya kwenye Visiwa vya Ziwa Viktoria.
“Kwa kipindi cha miaka kumi, MV. Jubilee Hope imekuwa msaada mkubwa kwa jamii, ikitoa huduma za afya kwa maelfu ya watanzania waliopo visiwani ndani ya Ziwa Viktoria, ambako huduma za afya zilikuwa na changamoto katika upatikanaji wake”.
Kupitia huduma hizi, tumeshuhudia mafanikio makubwa katika kupunguza magonjwa, kuokoa maisha, na kuboresha ustawi wa jamii kwa ujumla. Ameongeza Mhe. Mtanda.
Kadhalika Mkuu wa Mkoa amesema Uzinduzi wa MV. Lady Jean ni Hatua Mpya ya Maendeleo katika kuendeleza huduma za matibabu kwa wakazi wa Ziwa Viktoria.
Ambapo Meli hiyo mpya itaimarisha juhudi za huduma za afya kwa jamii ya visiwani kwa Kupanua wigo wa utoaji wa huduma za matibabu kwa idadi kubwa zaidi ya wagonjwa 7, Kuboresha utoaji wa huduma za dharura kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa zaidi.
“Hivyo, tunawashukuru sana kanisa la AICT kwa kuja na mradi wa Afya kupitia meli hii ya Matibabu ya MV. Lady Jean”.
Naye Askofu wa Kanisa la AICT Mussa Magwesela, amesema anaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wanaoupata kuanzia walipoanza rasmi shughuli za utoaji wa matibabu kwa njia ya Meli ambapo kwa takribani miaka 10 sasa tangu pale walipoanza rasmi mnamo mwaka 2015
Kadhalika amesema Kwa miaka kumi iliyopita, wanajivunia mafanikio kama vile Huduma za afya zimetolewa kwa zaidi ya watu 500,000 katika visiwa vya ziwa Viktoria kwenye utoaji wa chanjo, matibabu ya malaria, huduma za afya ya uzazi, upasuaji mdogo na huduma za afya ya kinywa na meno.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.