Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Afya) Prof. Tumaini Nagu amehitimisha rasmi mafunzo ya mwaka wa tathimini na Utekelezaji wa huduma za Afya na usafi wa mazingira katika Mikoa na Halmashauri Mkoani Mwanza.
Mafunzo hayo yaliyoanza julai 2 yamehitimiswa Leo julai 5, 2025 katika ukumbi wa rock city mall ambapo mafunzo hayo yenye Lengo la kutoa fursa, kutathimini hali ya afya katika mikoa na kuweza kubainisha maeneo yaliyofanya vizuri, maeneo yenye changamoto na sehemu zinazohitaji ubunifu.
Aidha, Pro. Nagu amewataka washiriki wote kutumia mafunzo hayo kuitendea haki kwa kutoa taarifa kamili na Sahihi kwa jamii Ili kuweza kupunguza magonjwa ya mlipuko, huku akiwataka kuwa kipaumbele kusemea maeneo yenye changamoto ili yaweze kupatiwa ufumbuzi mapema.
“ Mafunzo haya ya siku nne naimani tutayatumia vizuri, tuendelee kuhimizana kutoa taarifa kwa wakati Ili kudhibiti magonjwa ya mlipuko yasiendelee”. Amesema Nagu.
Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba ametumia jukwaa hilo kuomba waganga wakuu wengine pia kushiriki katika vikao vingine vijavyo kwa lengo la kushirikana na maafisa hao, huku akiwataka kwenda kusambaza kile walichojifunza kwa maana afua tiba ni muhimu Ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.
“Naaminii tukiendelea kufanya kazi kwa pamoja tutatoka wote katika afua za Afya na usafi wa mazingira”. Ameeleza Dkt. Jesca.
Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa mkutano wa mwaka wa tathimini ya utekelezaji wa huduma za afya na usafi wa mazingira katika mikoa na halmashauri Ndg. Seleman Yundo amewasihi washiriki kufuata sheria na taratibuu za wizara, na kuzingatia miiko na taratibuu zote za kazi kwa maslahi mapana ya jamii na Nchi kwa ujumla.
Mkutano huo mwenye lengo la kuwapa elimu na ujuzi maafisa Afya hao wa mikoa na halmashauri ulikuwa na kauli mbiu ya “utekelezaji wa afua za Afya na usafi wa mazingira NI msingi wa kinga endelevu dhidi ya magonjwa na Ustawi wa Jamii”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.