Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI (Afya) Prof. Tumaini Nagu amewasihi wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote ili kujihakikishia matibabu bora na haraka pindi wapatapo changamoto za kiafya.
Ametoa wito huo leo Julai 04, 2025 akiwa ofisini kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza alipofika kusalimia kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku mbili atakayoifanya Mkoani humo kwa ukaguzi wa miundombinu na huduma za afya.
Prof. Nagu amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya nchini kwa kutenga fedha nyingi kwenye ununuzi wa dawa, vifaa tiba pamoja na kuajiri wataalamu lakini jamii lazima ijenge utamaduni wa kuchangia gharama za matibabu.
“Serikali inawajali sana wananchu wake, zaidi ya Tshs. Bilioni 200 zinatolewa kila mwezi kuendesha sekta ya Afya, mathalani vifaa kama CT Scan ambazo zinahitaji umeme wakati wote na ukarabati wa vifaa tiba sasa kwanini wananchi wasiunge mkono kusaidia hilo.” Prof. Nagu.
Aidha, amezitaka hospitali za rufaa kuvilea vituo vya chini kwa kutoa mrejesho wa matibabu wanayoyatoa kwa wagonjwa waliowapokea na namna ya kuboresha mfumo wa mawasiliano ili kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinakomeshwa nchini.
Vilevile, amebainisha mpango wa serikali wa kuendelea kuajiri na kuboresha makazi ya watumishi wa sekta hiyo kuwa ni endelevu na akatoa wito kwa halmashauri kusaidia pia kwenye eneo hilo kwa kutukia mapato ya ndani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.