RAS MWANZA AWATAKA VIONGOZI WA UMMA KUDUMISHA NIDHAMU NA UFANISI KAZINI
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza ndugu Kusirie Swai amewataka viongozi wa umma kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma katika kusimamia nidhamu kwa watumishi katika ofisi zao.
Bwana Swai amesema hayo leo tarehe 26 Mei, 2025 wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Maadili kwa viongozi wa umma yaliyoandaliwa na Ofiai ya Rais Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma kwa kushirikiana na chuo cha uhasibu Arusha yaliyofanyika jmJijini Mwanza.
Amesema, maadili ni nguzo muhimu katika kuendeleza Taifa lolote kwani yanasaidia kujenga imani kwa wananchi juu ya watumishi wanaowawakilisha kwenye utumishi wa umma.
"Maadili yanasaidia kujenga tija na thamani ya rasilimali jinsi zinavyotumika kwa masilahi ya Taifa lao kama madini na maji kwa manufaa ya wote." Ndugu Swai.
Ameongeza kuwa palipo na maadili panaakisi uwajibikaji na uwazi na kufanya wananchi na viongozi kutoa mchango mkubwa na wa haraka katika kuendeleza nchi yao tofauti na sehemu yenye mmomonyoko wa maadili.
Aidha, amebainisha kuwa viongozi wakijikita katika kuhamasisha uadilifu inasaidia kuepusha mgongano wa maslahi na kuzuia rushwa na hulka ya ubinafsi kwa viongozi wa umma.
Katibu msaidizi kutoka Ofisi ya Rais sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma kanda ya ziwa Ndugu Goodson Kweka amebainisha kuwa mafunzo hayo ni programu maalum kwa viongozi wote wa umma ikiwa ni kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao.
"Mafunzo haya yatasaidia kukuza na kuendeleza maadili ya viongozi umma na yatasaidia kubadilishana uzoefu katika kuhakikisha sheria na miongozo ya maadili inafuatwa." Amebainisha Kamishna Kweka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.