RC MTANDA AIPOKEA BODI YA KITAIFA YA USHAURI NA MSAADA WA KISHERIA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 10 Februari, 2025 ameipokea na kufanya mazungumzo na Bodi ya Kitaifa ya Ushauri ya msaada wa kisheria iliyofika ofisini kwake kujitambulisha kufuatia ziara yao Mkoani humo.
Akizungumza mara baada ya kuipokea Bodi hiyo ofisini kwake Mhe. Mtanda ameiahidi bodi hiyo ushirikiano wanapotekeleza majukumu yao na akabainisha kuwa Mkoa huo unaamini kwenye usuluishaji wa migogoro nje ya mahakama kwa kusikiliza pande mbili za malalamiko.
Akizungumzia matukio kama ukatili wa kijinsia, amesema ofisi yake inashirikiana na jeshi la polisi kuyadhibiti na akatolea mfano utekaji wa watoto 2 juma lililopita kwenye shule ya Blessing ya Nyasaka wahalifu hao walishakamatwa.
"Sisi Mwanza tunaendelea na juhudi za kumaliza migogoro na kero za wananchi na hapa huwa tuna Open Court kwa kuwasikiliza pande mbili zinazolalamikiana, kesi nyingi tunazopokea hapa ni za mirathi na zinafuatiwa na migogoro ya ardhi na tumekua tukiwasikiliza na kutatua kero bila kuingilia mahakama." Mkuu wa Mkoa.
Makamu mwenyekiti wa bodi hiyo Mhe. Saulo Malauri amesema wamefika Mkoani Mwanza kwa ajili kusikiliza changamoto za kisheria katika kuangazia namna bora ya kumaliza kero na migogoro na kuhakikisha wanatekeleza sera ipasavyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.