• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

BARABARA MPYA YA LAMI KUCHOCHEA MAENDELEO KATA YA KIRUMBA-ILEMELA

Posted on: July 14th, 2023

*BARABARA MPYA YA LAMI KUCHOCHEA MAENDELEO KATA YA KIRUMBA-ILEMELA*


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023   Ndugu Abdalla Shaib Kaim leo Julai 14, 2023 amezindua barabara ya Lami Nzito na Zege Magomeni- Kirumba- Kabuhoro- Ziwani wilayani Ilemela yenye urefu wa KM 0.9 iliyojengwa na Mkandarasi Nyanza Road Works.

Akizindua mradi huo ndugu Kaim ameupongeza Uongozi wa Manispaa ya Ilemelaa kwa usimamizi madhubuti wa kazi iliyogharimu zaidi ya Milioni 998 hali iliyopelekea ubora unaotakiwa na viwango thabiti vilivyotarajiwa.

"Mradi upo vizuri na umezingatia viwango" amesisitiza kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru wakati wa uzinduzi baada ya kukagua barabara na kuridhika na ubora na viwango kutokana na thamani ya fedha iliyotumika.


Naye  Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha za Mradi huo kwani barabara hiyo imeondoka kero kubwa ya usafiri kwa wananchi wa kata ya Kirumba hasa wa kwenye makazi ya miinuko.

Katika wakati mwingine, Kiongozi wa mbio za Mwenge amewapongeza Ilemela kwa kutekeleza vema Ujenzi wa wodi ya wajawazito kwa zaidi ya Milioni 199 kwenye Kituo cha Afya Buzuruga ambapo shughuli ya Uzinduzi wa jengo hilo ilienda sambamba na ugawaji wa vyandarua kwa akinamama katika hatua za kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria.


Kabla ya kufika kwenye Mradi wa kugawa vifaa vya kufanyia usafi na zoezi la usafi kiloleli, Mwenge wa uhuru ulifika kwenye Shule ya wasichana ya Bwiru ambapo viongozi hao na wa wilaya walipanda miti ya matunda 3000 katika kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na lishe bora na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akahimiza utunzwaji.

Vilevile, Mwenge wa uhuru ulimulika mradi wa Vijana wa ufugaji kuku Nyasaka na ukapongeza Halmashauri kwa kuwapatia mkopo wa Milioni 15 kikundi hicho pamoja na kitoa elimu ya Ufugaji na wakatoa wito kwa Halmashauri kuwakopesha zaidi wakimaliza marejesho na mwisho ukaweka Jiwe la msingi kwenye Ujenzi wa Bweni la wanafunzi Buswelu shule ya msingi.

Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 inasema "Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa."

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti