Baraka ya Ufadhili Yamuangukia mtoto Gosbert
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe .John Mongella atoa ahadi ya kumugharimia mtoto Gozibeth Bwele mwenye miaka 10 elimu ya sekondari pindi atakapofanya vizuri katika matokea ya kujiunga na elimu hiyo.

Ametoa ahadi hiyo wakati akiitambulisha meli mpya ya Mv.Butiama hapa kazi tu ambayo imefanyiwa marekebisho makubwa baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya kazi alisema hayo baada ya kusikia mtoto huyo anayesoma darasa la tano anafanya vizuri katika masomo yake kwa kushika nafasi ya pili.

" Mtoto huyo ni mchezaji wa ngoma katika kikundi cha Utandawazi na ninamfahamu kwa kipindi kirefu lakini sasa amekuwa japo kuwa anacheza ngoma bado anafanya vizuri kuna watoto wengine awachezi ngoma lakini bado wanafanya vibaya katika masomo yao "alieleza Mhe. Mongella.
